Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bilionea Marinakis yupo sokoni kusaka kocha mpya Forest

FOREST Pict

Muktasari:

  • Mmiliki wa klabu hiyo, Evangelos Marinakis amemfuta kazi kocha wa tatu ndani ya msimu huu, na bado hata Siku ya Wapendanao (ambayo ni leo Jumamosi) ilikuwa haijafika.

LONDON, ENGLAND: SI jambo la kushangaza kwa wengi kwamba Nottingham Forest wanatafuta kocha mwingine.

Mmiliki wa klabu hiyo, Evangelos Marinakis amemfuta kazi kocha wa tatu ndani ya msimu huu, na bado hata Siku ya Wapendanao (ambayo ni leo Jumamosi) ilikuwa haijafika.

Hakutakuwa na mapenzi mengi kati ya pande hizo, hasa kwa Sean Dyche ambaye ndiye wa hivi karibuni kuondoka.

Hakuna kati yao anayetarajia salamu za heri wikendi hii baada ya kipindi kilichoonekana kama ndoto katika Uwanja wa City Ground kukatizwa mapema, baada ya mechi 25 tu.

Kwa bahati mbaya kwa Dyche, mzaliwa wa Nottingham, hali hiyo imeongeza hofu ya kushuka daraja kwa Forest.

Sare ya Jumatano dhidi ya Wolves iliwaacha Forest wakiwa pointi tatu mbele ya West Ham baada ya Manchester United kusawazisha dakika za mwisho dhidi ya Wagonga Nyundo hao wa London saa 24 baadaye, lakini vita vya kusalia Ligi Kuu England vimeanza rasmi.

Forest (nafasi ya 17) iko pointi mbili tu nyuma ya Tottenham (16) na tatu nyuma ya Leeds (15), na pointi nne kutoka Brighton (14). Hata hivyo, bado wanaangalia zaidi upande wa kushuka daraja kuliko kupanda.

Ushindi mara mbili katika mechi 10 (ingawa ni bora kuliko Spurs) haukutosha kuwanyamazisha mashabiki waliokuwa wakilalamika, hasa baada ya kupoteza pointi dhidi ya wapinzani wao wa karibu wiki za karibuni.

Ushindi dhidi ya West Ham mapema Januari unaonekana muhimu, lakini sare dhidi ya Crystal Palace na kipigo kutoka Leeds United kimekuwa mwisho wa safari ya Dyche.

Kuna kejeli kwamba timu yake, kwa namna fulani, ilipata “Dyche’d” katika mechi yake ya mwisho.

Forest walipiga mashuti 35 na kukusanya xG ya 2.55 (matarajio ya mabao) dhidi ya Wolves, idadi sawa na mashuti ya mechi nne zilizopita kwa pamoja.

Matokeo ya mwisho bado hayakubadilika kwa Marinakis. Sasa anageukia nani? Hawa hapa ni baadhi ya majina yanayozungumzwa.


FORE 01

Vitor Pereira

Kama huwezi kuwashinda, kwa nini usimwajiri kocha wao wa zamani? Kipindi cha Pereira, Molineux kilimalizika vibaya, lakini miezi 12 kabla yake aliiongoza Wolves kwenye “kupona kimiujiza”. Aliongoza Wolves kushinda mechi tano mfululizo karibu wakati kama huu msimu uliopita na kuwanusuru kushuka daraja. Alionekana akisherehekea na mashabiki kwenye baa za eneo hilo na haikuwa bahati tu.

Kocha huyo Mreno ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi kwa sasa, na ni rahisi kuelewa kwa nini. Rekodi yake imechafuliwa na msimu mbaya wa 2025-26, lakini kulikuwa na matatizo makubwa zaidi ya ndani na kwa miezi mitatu muhimu aliweza kuyadhibiti. Kwa sasa, hilo ndilo Forest wanahitaji.


FORE 02

Enzo Maresca

Baada ya kujaribu kocha mmoja mgumu anayeshikilia mbinu zake na aliyeshinda taji la Ulaya akiwa na klabu ya London msimu uliopita, kwa nini wasijaribu mwingine?

Maresca, kama wengine wengi kwenye orodha hii, yuko huru kwa sasa na ana wasifu mzuri nchini England. Swali ni kama Mtaliano huyo anaweza kuleta uthabiti Forest. Mtindo wake unaonekana kufaa zaidi timu zinazotaka kushambulia na kupigania nafasi za juu, si zile zinazopambana kushuka daraja.

Je, ana uwezo wa kuhimili vita halisi ya kushuka daraja? Na baada ya kuwa na mvutano Chelsea, je, ataweza kufanya kazi chini ya Marinakis, ambaye inasemekana ni mgumu zaidi?


FORE 03

Thomas Frank

Huenda kuna mashabiki wa Spurs ambao wasingejali Dyche achukue nafasi ya muda mfupi ili kuwaokoa kushuka daraja na hilo si mzaha kabisa. Lakini, ukweli ni kwamba Frank ana mengi ya kujivunia.

Hakuonekana kufaa katika klabu kubwa, lakini aling’ara Brentford ambako aliweza kucheza kwa mtindo wa kujibu mashambulizi na kufanikiwa. Swali kubwa ni kama yuko tayari kurejea kazini haraka baada ya mambo mgumu Tottenham na kama ataweza kufanya kazi katika mazingira ya misukosuko ya Forest. Brentford waliweka mfumo uliomfaa. Spurs hawakufanya hivyo.

Je, mafanikio yake yalitokana zaidi na mazingira aliyokuwepo? Na nini kitatokea bila muundo huo? Hofu hizi ni sahihi, ingawa anaweza kufanya kazi nzuri Forest. Kwa kuangalia nje ya Spurs, aliiboresha Brentford na kuwakuza wachezaji wengi. Forest inahitaji hilo kwa sasa, utulivu katika kipindi cha presha.


FORE 04

Roberto De Zerbi

Hili linaingia kwenye kundi la makocha wa Kiitaliano wenye tabia ya moto kama Maresca. De Zerbi ana uwezo mkubwa, anaweza kuifanya timu icheze soka la kuvutia na la kasi kwa muda mfupi.

Lakini je, hilo ndilo Forest wanahitaji sasa? Ange Postecoglou alijaribu kitu kama hicho na akashindwa vibaya. Forest haiwezi kumudu hatari hiyo katikati ya msimu. Labda wakisalia chini ya kocha wa muda, wanaweza kuwa na mipango mikubwa majira ya kiangazi. Lakini si sasa wakati hatari ni kubwa hivi. Zaidi ya hayo, De Zerbi ana historia ya kutofautiana na watu  jambo ambalo Forest hawahitaji kwa sasa.


FORE 05

Ole Gunnar Solskjaer

Baada ya kupoteza nafasi ya kuwa kocha wa muda wa Manchester United kwa Michael Carrick, je, Ole anaweza kushawishika?

Amewahi kupitia hali ya kutamba na kuteseka akiwa na Man United na Cardiff na pia yuko huru kwa sasa.

Hata hivyo, itakuwa ni hatua ya kurudi nyuma kulinganisha na matarajio yake ya awali na ukosefu wa uzoefu wa hivi karibuni unaweza kumweka kwenye mazingira magumu katika kipindi hiki kigumu cha msimu.