Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah kuchukua nafasi ya Benzema Al-Ittihad

Muktasari:

  • Taarifa zinasema kuwa, staa huyo yuko tayari kujiunga na wababe hao wa Saudi Arabia ikiwa makubaliano yatafikiwa

BAADA ya kuachana na Karim Benzema aliyetimkia Al Hilal, sasa Al Ittihad imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah (33) katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Taarifa zinasema kuwa, staa huyo yuko tayari kujiunga na wababe hao wa Saudi Arabia ikiwa makubaliano yatafikiwa.

Salah amekuwa akiwindwa na klabu za Saudi Arabia kwa zaidi ya misimu miwili sasa, lakini safari hii Al-Ittihad inaonekana kuwa tayari kuvunja benki ili kumsajili nyota huyo.

Kwa sasa Salah bado ana mkataba na Liverpool unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote, amefunga mabao sita na kutoa asisti sita.

Alikuwa akitajwa sana kwamba huenda angeondoka katika dirisha lililopita la majira ya baridi baada ya kuzuka kwa sintofahamu kati yake na kocha Arne Slot.

Salah alitamka hadharani kwamba haoni kama ana maisha marefu Liverpool na akadai kuwa benchi la ufundi limekuwa likimwangushia yeye jumba bovu kutokana na matokeo ambayo timu ilikuwa inayapata.

Hiyo ilisababishwa aondolewe katika timu kwa muda na akakosa mechi kadhaa kabla ya kukutana na Slot na kumaliza tofauti zao.

Hata hivyo, ripoti zinadai Salah bado anahitaji kuondoka kwani anaamini ni muda wa kupata changamoto mpya sehemu nyingine.


Morgan Gibbs-White

ASTON Villa imejitosa katika kinyang'anyiro cha kuiwania saini ya kiungo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, Morgan Gibbs-White, 26, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Taarifa zinaeleza kuwa Nottingham ipo tayari kumuuza staa huyo endapo itapewa ofa kubwa, jambo linaloashiria uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka katika dirisha lijalo.


Harry Maguire

BEKI wa kimataifa wa England, Harry Maguire, 32, anaonekana kuwa karibu zaidi kusaini mkataba mpya na kuendelea kuitumikia Manchester United wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Licha ya kuwa na panda shuka nyingi, Maguire bado anaaminiwa na benchi la ufundi la Man United kutokana na uzoefu wake.

Katika mkataba huo mpya Man United inataka kupunguza mshahara tofauti na ule ambao anaupata kwa sasa.


Cristian Romero

REAL Madrid imeanza msako wa beki mpya wa kati na jina la nahodha wa Tottenham Hotspur, Cristian Romero, 27, raia wa Argentina, limeibuka kama moja ya machaguo yao.

Romero ameendelea kung ara katika Ligi Kuu England akiwa na Spurs, licha ya timu hiyo kutokuwa na mwenendo mzuri kwa msimu huu.

Mbali ya Madrid, Romero anawindwa pia na Barcelona na Atletico Madrid.


Harry Kane

BAYERN Munich imeanza rasmi mazungumzo na mshambuliaji wake wa kimataifa wa England, Harry Kane, 32, kuhusu mkataba mpya na mabosi wa timu hiyo wana imani kuwa staa huyo atakubali kusaini.

Kane amekuwa nguzo muhimu kwa Bayern tangu alipojiunga akitokea Tottenham Hotspur, akivunja rekodi kadhaa za mabao ndani ya Bundesliga.

Uongozi wa Bayern unamwona Kane kama sehemu ya mradi wa muda mrefu wa klabu hiyo.


James Trafford

LEEDS United inaandaa ofa ya Pauni 30 milioni kwa ajili ya kumsajili kipa wa Manchester City na timu ya taifa ya England, James Trafford, 23, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Trafford, ambaye amekuwa akitafuta nafasi ya kucheza mara kwa mara, anaonekana kuvutiwa zaidi na ofa ya Leeds ambayo imehakikishia nafasi ya kuwa kipa namba moja.

Manchester City ipo tayari kusikiliza ofa, kutoka kwa timu itakayohitaji kumnunua lakini inataka kuwepo kwa  kipengele cha kuwa wa kwanza kumnunua ikiwa Leeds itataka kumuuza.


Jean-Philippe Mateta

CRYSTAL Palace inaweza kupunguza bei ya awali ya Pauni 30 milioni iliyokuwa inahitaji ili kumuuza mshambuliaji wake wa kimataifa wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta mwenye umri wa miaka 28, katika dirisha lililopita la majira ya baridi.

Staa huyu anawindwa na Man United ambayo imeonyesha wazi kwamba inahitaji huduma yake katika dirisha lijalo.

Katika dirisha la Januari mwaka huu, Mateta alikuwa tayari kujiunga na Juventus kabla ya dili kufeli katika dakika za mwisho baada ya kocha Oliver Glasner kuzuia asiuzwe.


Sandro Tonali

JUVENTUS pamoja na klabu nyingine za Serie A zinafikiria kuachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Newcastle United, Sandro Tonali katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Changamoto inayoonekana kuwarudisha nyuma vigogo wengi wa Italia ni mshahara mkubwa ambao staa huyu anadaiwa kuuhitaji.

Tonali mwenye umri wa miaka 25, alitajwa kutaka kuondoka pia Januari, lakini alisitisha na kusisitiza kwamba atabaki hadi mwisho wa msimu huu ili kuona kama Newcastle itafuzu michuano ya kimataifa au laa kabla hajafanya uamuzi.