Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BAB'KUBWA… 33 WPL mzigoni WAFCON 2026

WPL Pict

Muktasari:

  • Katika michuano hiyo iliyopigwa wikiendi iliyopita, nyota wa ligi kuu walikiwasha kwenye mataifa yao wakiwamo wa Simba Queens, Yanga Princess na JKT Queens na kuweka heshima katika mechi hizo.

LIGI Kuu ya Wanawake (WPL) imesimama kwa mwezi mmoja kupisha timu za taifa zinazowania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wanawake (Wafcon) 2026 zitakazofanyika Morocco.

Katika michuano hiyo iliyopigwa wikiendi iliyopita, nyota wa ligi kuu walikiwasha kwenye mataifa yao wakiwamo wa Simba Queens, Yanga Princess na JKT Queens na kuweka heshima katika mechi hizo.

Nyota wa JKT, Stumai Abdallah na Donisia Minja ni kati ya wachezaji walioipeperusha vyema Bendera ya Taifa kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Equatorial Guinea na Twiga Stars ilishinda mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Hapa mwanaspoti linakuchambulia nyota 33 wa ligi kuu wanaokiwasha kwenye michuano hiyo ya kufuzu Wafcon na wanatarajiwa pia kukiwasha wiki hii kwenye michezo ya pili ya kuvuka kwenda hatua inayofuata.

WP 01

1. TANZANIA (16)

Twiga Stars imebakisha hatua moja tu kuvuka kwenda raundi ya pili na katika kikosi chake, kuna nyota 16 walioko ligi kuu huku JKT Queens ikiongoza kwa kutoa wachezaji 10, Simba wanne, Fountain Gate wawili, huku Yanga, Mashujaa Queens na Bunda Queens zikitoa mmoja kila moja.

Nyota hao 10 wa JKT kipa Naijat Abbas ambaye ndio kipa namba moja wa wanajeshi hao akiwa na clean sheet nane, beki wa kulia, Lidya Maximilian ukiwa msimu wake wa pili JKT, kiungo Donisia Minja miongoni mwa wachezaji wa wakongwe ambao ni wazuri wa kupiga mipira ya faulo na penati hadi sasa akiwa na mabao matano, beki Anastazia Katunzi waliomaliza dakika 90, Stumai Abdallah aliyeingia kipindi cha pili na kufunga bao moja na ndio kinara wa mabao ligi kuu akiwa nayo 18.

Wengine ni Elizabeth John ambaye ni msimu wake wa kwanza kucheza JKT na ndio mara ya kwanza kucheza Stars kwa dakika 49, beki Christer Bahera ambaye ligi kuu alicheza mechi 11, Winifrida Gerald waliocheza dakika 28 na ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri ligi kuu akiwa na umri wa miaka 17 amefunga mabao saba, beki Janeth Pangamwene, kiungo Joyce Lema na mshambuliaji Jamila Rajabu wote wakikaa benchi na kwenye timu yao wamekuwa wakicheza na kuonyesha kiwango.

Simba iliwakilishwa na kipa Janet Shija ambaye amedaka mechi zote 12 msimu huu akiwa mbadala wa Carolyne Rufaa ambaye atakaa msimu mzima kutokana na majeraha, Ester Mayala na Violeth Nickolaus  ndio mabeki pekee waliyocheza dakika nyingi 1080 na kwenye mchezo wa juzi walianzia benchi.

Aisha Mnunka aliyecheza dakika 45 akianza msimu kwenye duru la pili baada ya kukaa nje kwa takribani nusu msimu akiwa na mgogoro na timu yake uliyomalizwa hivi karibuni na Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Fountain Gate waliokuwepo ni Marry Siyame na Winifrida Charles washambuliaji ambao ndio panga pangua wa kikosi hicho, Yanga ni Asha Ramadhan ambaye amekuwa akisugua benchi, Mashujaa ikitoa kipa mmoja Asha Mrisho ligi kuu ameruhusu mabao 12 na Bunda ni  Ester Maseke anayecheza eneo la kiungo wa chini.

WP 02

2. KENYA (6)

Kenya maarufu kama Harambee Starlets haijaanza vizuri kampeni hizo kwa raundi ya kwanza na ilikubali suluhu dhidi ya Tunisia nyumbani.

Nyota walioiwakilisha nchi hiyo kutoka ligi kuu watano wanatoka Simba Queens ambao ni Jentrix Shikangwa (Simba) na anashika nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa na mabao 17, mabeki Ruth Ingosi na Wincate Kaari ambao wote wawili wanacheza eneo la pembeni kwenye kikosi cha mnyama.

Wengine ni Elizabeth Wambui na Vivian Corazone ambao wanamchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba wakichangia mabao 10 hadi sasa huku Lydia Akoth ambaye alisajiliwa na Yanga dirisha dogo akitokea nchini Kenya na kucheza mechi mbili tu.

Kati ya wachezaji hao watatu tu ndio walianza kwenye mchezo huo, Corazone, Wambui na Ingosi huku Shikangwa akiingia kipindi cha pili.

Nyota hao ni wachezaji wazoefu kwenye ligi ya Tanzania kwa msimu wa tatu mfululizo wakiwa ndio wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba.

WP 03

3. ETHIOPIA (2)

Ilikubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Uganda ugenini huku nyota wa ligi kuu waliotumikia ni wawili, Aregash Kalsa na Ariet Udong na wote wanakipiga Yanga na walisajiliwa kutoka C.B.E ya nchini kwao.

Kalsa ndiye mchezaji pekee aliyecheza kwenye mchezo huo, huku Udong ambaye licha ya kuitwa kwenye kikosi alisalia Tanzania kwa uangalizi maalumu wa madaktari kutokana na jeraha la goti alilolipata mwezi uliopita kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Bunda Queens.

Kalsa alitambulishwa na Yanga hivi karibuni akitokea C.B.E ambako alinyakua ndoo ya michuano ya CECAFA kwa wanawake wakiitandika bao 1-0 Kenya Police.

Hadi sasa Kalsa amecheza mechi tatu dhidi ya Alliance, Bunda na Mashujaa timu yake ilipoondoka na pointi tatu huku akifunga bao moja kwenye mechi hizo.

Uwepo wake umeongeza kitu kwenye kikosi cha Yanga ambacho kilikuwa na changamoto ya kiungo mshambuliaji wa kutengeneza nafasi kwa washambuliaji.

Mara ya mwisho nyota huyo kuitwa kikosi cha timu ya taifa ilikuwa 2022 tangu hapo amekuwa akishuhudia timu ya Ethiopia na mechi tatu mfululizo alizoonyesha kiwango bora kimemrudisha tena kikosini.

WP 04

4. UGANDA (1)

Tausi FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ndiyo imetoa nyota mmoja raia wa Uganda, kipa Aturo Ruth na alicheza dakika zote 90 akiondoka na clean sheet.

Hii ni ishara njema kwa Ligi daraja la kwanza hapa nchini kwani imekuwa kiasi cha mchezaji wa ligi hiyo kuitwa kwenye kikosi kilichosheheni nyota wakubwa.

Alitambulishwa kwenye kikosi cha Tausi FC  siku chache zilizopita akitokea Al Shabab inayoshiriki Ligi Kuu Saudia ambako alicheza mechi mbili tu ndani ya misimu miwili tangu aliposajiliwa 2022.

Ndio kipa tegemeo wa Uganda kwani alishawahi kucheza mashindano mbalimbali ikiwemo COSAFA Championship ya mwaka 2021.

WP 05

5. ZIMBABWE-1

Timu hiyo juzi ilipoteza mchezo kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya Angola, ikiwa ni miongoni mwa michezo mikali uliyoshuhudia wiki iliyopita.

WPL imetoa mchezaji mmoja, Danai Bhobho anayekipiga Yanga Princess akiwa ni nyota pekee kutoka ligi kuu kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa.

Bhobho anaingia kwenye kitabu cha nyota wa kigeni waliocheza timu za Kariakoo kwani kabla ya Yanga aliwahi kuitumikia Simba.

Beki huyo wa pembeni ambaye pia ana uwezo wa kucheza kiungo wa chini amekuwa na mfulilizo wa kuitwa kwenye kikosi cha taifa cha Zimbabwe kutokana na kiwango chake.

Hadi sasa Bhoho amecheza mechi 11 za ligi akiwa na Yanga msimu huu tofauti na ana mataji mawili ya ligi akiwa na Simba mwaka 2021 na 2023.

WP 06

6. MALI -1

Mali ni miongoni mwa nchi zilizoendelea kwenye soka la wanawake ingawa ligi yao haina ushindani mkubwa lakini ina vipaji vingi vya wachezaji wa kike na kiume.

Fatoumata Diarra wa Tausi FC ya Ligi Daraja la Kwanza alicheza dakika zote 90 dhidi ya Gabon kwenye ushindi wa mabao 6-0 huku akiingia kambani mara mbili.

Ndio kapteni wa kikosi cha Mali na alitambulishwa hivi karibuni na Tausi akitokea Mande ya nchini kwao.

Hii sio mara ya kwanza kwa nyota huyo kulitumikia taifa lake kwani mwaka 2004 alicheza mechi tano za kufuzu WAFCON  na kufunga mabao matatu.

Mshambuliaji huyo (38) aliifungia tena Mali mabao matatu kwenye michuano hii mwaka 2018 jambo ambalo limekuwa na muendelezo kwake na msimu huu tayari kafunga mabao mawili kwenye mechi moja.

WP 07

7. BURKINA FASO - 1

Nyota Adama Congo huyu anayejiunga na Tausi FC anaiwakilisha timu ya taifa ya Burkina Faso.

Hii si mara ya kwanza kwa Congo kuitwa timu ya taifa mara ya mwisho aliifungia timu yake bao moja kwenye fainali za mashindano hayo mwaka 2022 dhidi ya Morocco.


RATIBA ILIVYO

Feb 26, 2025

Tanzania v Guinea ya Ikweta (Estadio de Malabo, Malabo)

Burkina Faso v Burundi (Stade du 26 Mars, Bamako)

Tunisia v Kenya (Sousse Olympic Stadium, Sousse)

Mali v Gabon (Stade du 26 Mars, Bamako)

Ethiopia v Uganda (Abebe Bikila Stadium, Addis Ababa)