Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI aanika sababu tatu zinazoibeba Yanga

AZIZ KI Pict


JANA katika sehemu ya pili ya makala ya Stephanie Aziz KI aliyefanya mahojiano maalumu na Mwanaspoti, alianika jinsi alivyomnasa mwanadada Hamisa Mabetto hadi kumuoa na kumuelezea jinsi alivyo tofauti na anavyotazamwa nje na wanajamii.


Aziz KI pia alifunguka jinsi wanavyoishi kama wanandoa na jinsi alivyowekewa bonasi kila anapofanya vyema uwanjani, mbali na kufurahia kuondolewa kwa Fadlu Davids katika klabu ya Simba na sababu zake.


Leo tunamalizia makala haya ya kiungo mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Wydad Casablanca, akiweka bayana namna anavyoiona Yanga ikizidi kufanya vyema zaidi katika ligi ya ndani na anga za kimataifa. Kwa sababu gani? Endelea naye...!

AZI 02

YANGA ITASUMBUA SANA

Aziz KI aliyeitumikia Yanga kwa misimu mitatu tangu ilipomsajili kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast na kushinda nayo mataji mbalimbalio ikiwamo na yeye kuwa Mfungaji Bora na Mchezaji Bora (MVP) anasema;

“Nimekaa Yanga kwa miaka mitatu ya maisha mazuri, nilipokewa vizuri na wananchi nikaishi nao vizuri sana, tulipofungwa na hata tulipopoteza tulikuwa pamoja, naweza kusema ni klabu ambayo imechukua nafasi kubwa kwenye moyo wangu kwa namna nilivyokaa nayo muda huo hapa Tanzania.”

Anapoulizwa kama anaiona Yanga ikiendelea kuwa na moto kama enzi akiitumikia, anajibu;

“Kwanza lazima ufahamu mimi ni Mwananchi, nitaiombea mema wakati wote na nitaisapoti kwa sababu nilikuwa hapa ni furaha kuwa sehemu ya hii klabu.

“Nimetengeneza familia hapa, nina heshima kubwa na rais wa klabu (Hersi Said) GSM mwenyewe (Ghalib Said Mohammed), mke wake  na kila mtu kwenye ofisi ya klabu hii, hivyo kwangu sio suala la kufikiri ni kuiombea Yanga iendelee kufanikiwa zaidi na hilo linanipa furaha kubwa.

“Mimi nikiona mashabiki wa Yanga wana furaha nami nikiwa mmoja wao, nikiona wameshinda taji kiukweli ni kitu kizuri sana kwangu. Hivyo basi naamini itaendelea kufanya vizuri, nawaamini viongozi wake na mipango yao mikubwa, lakini naamini juu ya ubora wa timu,” anasema Aziz KI na kuo-ngeza;

“Zipo sababu za kuamini Yanga itaendelea kusumbua, kwani ina wachezaji bora na wenye kujua wanachokifanya uwanjani. Ina uongozi bora unaosimamia mambo kwa ufanisi, lakini hata benchi la ufundi naona linafanya kazi nzuri na ukiunganisha na mshikamano kwa wanachama, mashabiki na wapenzi ni wazi hakuna cha kuizuia kuendelea ilipoishia. Wataendelea kufanikiwa.”

AZI 01

MAISHA YAKE NA HERSI

Ukifurahia uwapo wa Aziz KI basi hapohapo unatakiwa kutambua kazi aliyofanya rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa namna ambavyo alipambana kumshawishi kiungo huyo kuja kujiunga na timu hiyo hapa anaeleza namna walivyoshibana.

“Kama unaweza kuona mtu zaidi ya wakala wa wachezaji, akaamua kunifuata kwetu nyumbani Ivory Coast kuzungumza nami Hersi alifanya hili, watu wanaweza kupigia simu na kuzungumza nawe wanapokuhitaji, lakini kwake (Hersi) ilikuwa tofauti, alinifuata kama mara tatu kwa nyakati tofauti kunishawishi nijiunge na Yanga, mara ya kwanza ilikuwa tulipokuwa tunacheza na RS Berkane wakati huo nikiwa naitumikia ASEC Mimosas kule Morocco.

“Mara ya pili ilikuwa kule Ivory Coast akakutana na familia yangu, Sio rahisi kumuona mtu anakupa heshima kama hiyo ni zaidi ya rais kwangu, hata nilipofika hapa alikuwa ni kama mtoto wake, alinifanya niwe sawa kufanya kazi yangu hapa.

“Nikikumbuka wakati nafika hapa haikuwa rahisi kwangu kuzoea, nilikuja nikiwa na jina kubwa kwahiyo kila mmoja alikuwa na matajiro makubwa na mimi, wakati wote alikuwa karibu na mimi na sio yeye peke yake kila mmoja hapa alikuwa karibu na mimi.

“Alinipa hii nafasi kuja Tanzania alitengeneza nafasi kwa Watanzania kujua Aziz KI ni nani, kwahiyo nilikuwa nafuraha hapa ndio maana mliona hata nilipooa alikuwa mbele kufanya kila kitu, alisimamia kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho.”€

AZI 07

RUHUSA YA KUSIMAMIA NDOA

Wakati Aziz KI anaoa yaliibuka maneno kwamba Hersi alichukua jukumu la wanafamilia wa mchezaji huyo kusimamia ndoa hiyo, hapa Aziz KI anaeleza mambo yalivyokuwa.

“Hapana, ruhusa ya kusimamia kwake kila kitu ni mimi nilimpatia, nilifanya hivyo kwa kuwa alikuwa ni mtu ambaye wakati wote alinisapoti, alinipa ushauri, anajua kila kitu kilichotokea kimafanikio kwenye maisha yangu hapa.

“Tanzania msingi ni yeye, alinifungulia njia ya hayo yote kwasababu kama Hersi asingekuja nchini kwetu na kusema anahitaji nije kucheza Tanzania sidhani kama haya yote yangetokea, kwangu mimi mtu ambaye anakufungulia mambo kama hivi alivyofanya ni lazima nimlipe mema yake, yeye kuwa mbele katika harusi yangu lilikuwa jambo ambalo limenipa amani sana.”€


YANGA IKIYUMBA NAUMIA

“Yanga wanatakiwa kuendelea kufanya vizuri kwasababu wasipofanya vizuri, unajua mimi sasa sio mchezaji wa Yanga ni shabiki wao.

“Unajua mashabiki siku zote ni watu wa kulalamika, hawana furaha wakati timu inapoteza hata pale timu haichezi vizuri, kwangu mimi wanatakiwa kuendelea kufanya vizuri, wanatakiwa kila wakati kujitoa kwa asilimia mia moja ili washinde na wawe juu ya msimamo, hicho ndio kitu pekee kitakachonifanya niwe na furaha.”


PACOME, DOUMBIA NA YAO

Aziz KI anaeleza namna anavyotaka kuona Yanga inaendelea kutamba lakini kumbe haishii kuhitaji hilo tu anazungumza sana na wachezaji wenzake hasa Pacome Zouzoua, Mamadou Doumbia, Yao Akouassi na wengine akiwasisitiza haya:

“Naongea nao sana kila wakati, huwa nawaambia ukweli, hata kama nipo Morocco bado naangalia sana mechi za Yanga, huwa nawapigia, hata rais (Hersi) huwa nampigia naye na kumshauri eneo hili na hili hapana au hapa mnaweza kufanya vizuri na anaweza kuongea na wachezaji na wachezaji nao huwa naongea nao sana niwape sapoti yangu.

“Nafanya hivyo kwa sababu unajua soka huwezi kufanya kila kitu ukiwa mwenyewe unahitaji watu pia kukusapoti, unahitaji watu wanaoweza kukwambia ukweli, kwangu mimi najisikia faraja nilipokuja hapa Tanzania nikafungua milango ya wengine kuja na watu hapa wakaheshimu watu wa Ivory Coast na hata Burkina Faso.”

AZI 03

HATA MASTAA WA SIMBA

“Kwangu huwa nafurahi kila mchezaji anayekuja nyuma yangu afanye vizuri na hili sisemi kwa wachezaji wenzangu ambao wako Yanga pekee, lakini pia hata wale waliopo na Chamou (Karaboue) na SimbaAhoua (Jean) huwa nao naongea nao na kuwasisitiza juu ya kujituma wapo wengine pale Singida Big Stars na hata mdogo wangu mmoja yupo Azam wote huwa nazungumza nao kuwakumbusha namna ya kupambana.

“Unajua soka sio uadui, mnaweza kuwa timu tofauti mkashindana vikali uwanjani lakini bado mkawa kitu kimoja baada ya dakika 90, bado nyie ni familia moja kwahiyo hawa ni familia yangu wote na nina furaha kuwa nao pamoja na wananisikiliza na kunipa heshima.”€


KIWANGO CHA PACOME

“Bado mnaweza kuona mazuri zaidi ya anachofanya sasa (Pacome) kwa sababu kuanzia siku ya kwanza alipokuja hapa alionyesha ana ubora mkubwa.

“Kuwa bora hakuhitaji ufanye vizuri kwenye mechi moja au mbili unatakiwa ufanye kila wakati kwenye kila mchezo na anaweza kufanya hivyo namfahamu, namtakia kila la kheri najua akiendelea kufanya vizuri anaweza kupata mafanikio kama ambayo mimi niliyapata hapa, uwezo huo anao.”


ADO ADO ZA DOUMBIA, ECUA

Mastaa wengine wa Yanga ambao Aziz KI anafahamiana nao ni Doumbia na Ecua na anaeleza namna walivyoanza taratibu kikosini.

“Soka kila unapokwenda wakati mwingine kuzoea mazingira kunaweza kuja haraka au kukachelewa, hata mimi wakati nafika hapa sikuanza kwa presha kubwa nilianza taratibu sana.

“Nilihitaji muda kidogo kuanza kuonyesha ubora wangu, huwa nawaambia soka la Tanzania sio rahisi, kwa hiyo huwa nawakumbusha unapofika hapa usione kwa kuwa unaichezea timu kubwa mambo yatakuwa rahisi, nafikiri baada ya muda wakiendelea kujituma watazoea na kuonyesha kile kikubwa walichonacho.”

Kama kuna siri Aziz KI amewapa mashabiki wa Yanga ni hii kwamba yeye ndiye aliyempendekeza Doumbia kusajilwa na timu hiyo wakati yeye alipokuwa anajiandaa kuondoka nchini.

“Doumbia ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee sana, ndio sababu mimi nilimpendekeza asajiliwe Yanga kwa kuwa namfahamu, watu wanaweza kuona yuko taratibu, lakini anajua kucheza mpira, ni hatari sana.

“Kama akishazoea mazingira, ana akili sana akiwa uwanjani hasa kwenye pasi zake, anaweza kuitengeneza mechi, sijamjua kwa muda mfupi namfahamu kwa miaka mingi, watu watakuja kusahahu haya yote akianza kucheza kwa kiwango chake, huwa naongea naye sana kumsisitiza afanye mazuri.”€

Kumekuwa na mtazamo kwamba usajili wa Doumbia na Ecua kuwa ni mbovu, lakini Aziz KI anakataa kwa kusema;

“Huo ni mtazamo wa watu, kwenye soka kama unajua ni unajua tu, hawa ni wachezaji wenye ubora mkubwa bahati mbaya wameanza kwa nguvu ya chini, huwezi jua labda kuna kitu kimewapata au hawako sawa kuna mambo mengi sana kwenye safari ya kutafuta ubora wako.

“Kitu ninachoweza kuwaambia mashabiki ni kuwa wavumilivu wawape muda na nguvu wachezaji hao kuonyesha kile ambacho nakifahamu kwao.

“Huwa naongea nao sana, nawakumbusha hii ni Yanga ni moja ya timu kubwa hapa Tanzania, kwahiyo unapoichezea unatakiwa kutambua utakutana na presha kubwa, wanatakiwa kutafuta namna ya kuibeba hiyo presha isiwaharibie na wacheze vizuri, hapa hata kama utafunga hat trick leo na umecheza vizuri lakini watu wataongea juu yako.”

AZI 05

VIPI KUHUSU AHOUA?

“Mimi namuamini Ahoua, nadhani anaweza kurudia kiwango chake bora, itategemea yeye mwenyewe anataka nini, kitu ambacho watu wanatakiwa kuelewa msimu uliopita ametumia nguvu kubwa sana, amecheza mechi nyingi na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa.

“Labda msimu huu ameanza kwa kukabiliana na uchovu, inawezekana aliamini akifanya vizuri anaweza kupata nafasi nyingine mbali lakini akajikuta bado yuko hapa, kwa hiyo anatakiwa kujengwa kisaikolojia, hiyo ni kawaida kumtokea mchezaji yeyote.”


KUWEKEZA TANZANIA

“Hapa Tanzania ni nyumbani kwangu, nimeoa hapa na moja ya vitu nataka kufungua hapa kwanza ni kuanzisha taasisi yangu binafsi ambayo itakwenda kuwasaidia watoto na watu mbalimbali nimeshaanza kufanya mambo taratibu lakini pia nataka kufungua akademi hapa ya kutengeneza vipaji vya wachezaji wakubwa wa baadaye. Ukimuangalia Feisal Salum ‘Fei Toto’ unajua Tanzania ina vipaji sana.”

“Ukianzia chini kwa miaka 15 utapata wachezaji wazuri sana ambao watakuja kuichezea Taifa Stars baadaye.

“Unajua ukiamuangalia Fei Toto unaona kwamba mbali na kipaji chake, lakini aliandaliwa vizuri kutoka chini, malezi ambayo hata mimi niliyapata, unamuona namna anavyoweza kusogea na mpira na kuamua mambo, hayo yote wanatakiwa kupewa watoto kuanzia chini ili wakikua waendelee nayo.

“Mtoto lazima apewe mazoezi mazuri yanayostahili lakini pia apate elimu ya shule ili kumjenga maana kuna maisha baada ya soka, anatakiwa kujengwa kiakili ili mambo ya kuwa mchezaji mkubwa na umaarufu usimsumbue akaharibikiwa.”

AZI 09

KUMUDU DABI YA KARIAKOO

“Mimi siku zote huwa sitaki presha iniingie ninapokuwa uwanjani, kwa hiyo kwanza napenda kufanya vizuri kwenye mechi kubwa.

“Najua furaha ya mashabiki ninaowapigania ipo hapo, ni kweli mechi zilikuwa ngumu lakini kutokana na ubora wetu kama timu Yanga ilikuwa inaweza kushinda na haikuwa vigumu kwangu kufanikisha timu yangu kushinda.”