Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asanteni Masheikh, Maaskofu kwa kumwaga baraka Taifa

Muktasari:

Hawa si viungo asilia na mara nyingi wamekuwa mzigo katika nafasi ya kati kwa sababu si wanyang’anyaji wa mipira na akili yao imetengenezwa katika ushambuliaji zaidi.

JUMAPILI iliyopita, Oktoba 12 Alasiri ndani ya Uwanja wa Taifa kulikuwa na mkusanyiko wa viongozi wa dini zetu kuu za Waislamu na Wakiristo ambao walicheza mechi kwa kugawanyika katika timu mbili za Amani na Mshikamano.

Wakiwa katika timu hizo walicheza mechi iliyokuwa na lengo la kuhimiza umoja wetu Watanzania bila kujali imani ya mtu.

Hii imekuja baada ya kuonekana kwamba kuna vuguvugu linaloashiria kuzuka kwa mgawanyiko mkubwa katika jamii yetu.

Kizuri katika mechi hii ni kwamba waliocheza ni watu wa madhehebu yanayomwakilisha Mungu, walicheza katika uwanja ambao watu wa imani za kishirikina wamekuwa wakila pesa za viongozi wa soka na kuja hapo kuharibu utulivu wa uwanja wetu.

Wameshauchafua sana huku timu zao hizo zinazotumia imani hizo zikifungwa ingawa viongozi huwa hawaachi ushirikina wa mpira, Masheikh na Maaskofu wamehitimisha hilo baada ya kucheza mchezo ambao kwangu umerudisha baraka katika uwanja wetu.

Sina shaka kwamba baraka zao ziliambatana na mvua kidogo iliyonyesha kiangazi hiki tofauti na muda wake.

Ni wazi haimaanishi ushindi walioupata Taifa Stars ulitokana na baraka za wakuu wetu wa dini moja kwa moja ushindi huu umekuja vizuri tu kutokana na uungwana alioufanya kocha Mart Nooij wa kusikia mawazo ya wadau wengi.

Kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakilalamikia mfumo na mbinu ambazo Nooij amekuwa akitumia.

Tumeshuhudia mara nyingi tu jinsi wachezaji wa kati wa Stars walivyokuwa wakipata tabu pindi walipocheza na timu zilizokuwa zinajaza wachezaji wa katikati huku kocha wetu akiwatumia viungo asilia wawili na labda akiwatumia wachezaji wa pembeni kama kina Mrisho Ngassa, Haruna Chanongo, Simon Msuva na kidogo Ramadhani Singano.

Hawa si viungo asilia na mara nyingi wamekuwa mzigo katika nafasi ya kati kwa sababu si wanyang’anyaji wa mipira na akili yao imetengenezwa katika ushambuliaji zaidi.

Lakini kibaya zaidi ilikuwa ni matumizi ya wachezaji wengi wanaocheza katika nafasi ya ushambuliaji, tuliongelea sana pale alipokuwa akiwatumia kwa pamoja Mbwana Samatta,Thomas Ulimwengu, John Boko na Mrisho Ngassa.

Kwa wafuatiliaji wa michezo miwili tuliyocheza dhidi ya Zimbabwe na Msumbiji tulifungwa mabao matatu kati ya sita tuliyofungwa na timu hizo mbili yaliyofanana sana.

Mabao hayo yalitokana na muda ambao wachezaji wetu wa nafasi ya ushambuliaji walipopoteza umakini na mipira iliponyang’anywa na kufungwa kirahisi.

Kuna faida moja tu kubwa ambayo kocha anaweza kuipata iwapo wachezaji aliowapanga mbele wana uwezo wa kukaa na mipira kwa muda mrefu bila kunyang’anywa, hata ikitokea wamenyang’anywa isiwe wakati timu karibu yote imefunguka kwa kushambulia, lakini tuliona jinsi Wazimbabwe walivyopata bao lao hapa na Msumbiji walivyofika golini kwetu haraka.

Tunashukuru baraka za Masheikh na Maaskofu ziliambatana na ubadilishaji wa mfumo wa uchezaji kutoka kwa Nooij baada wa kuamua kuwatumia wachezaji watatu nyuma huku wachezaji viungo watano wakiwa katikati na kuwachezesha washambuliaji wawili mbele.

Huu ni mfumo ambao umekuwa ukitumiwa na timu zilizo na beki za pembeni zinazoweza kushambulia kila mara lakini wakiwa na majukumu ya kurudi mara moja pindi wanapopoteza mipira, mfumo huu wa 3:5:2 uliowahi kuipa mafanikio sana timu ya nyumbani hapa ya Ruvu JKT achana na hizo nyingi za Ulaya kama Real Madrid, Ajax na nyinginezo.

Nguvu ya mfumo huu inalindwa na uwezo wa beki za pembeni katika kujenga mashambulizi ya mara kwa mara.

Ilikuwa rahisi zaidi kwa Stars ilivyokuwa ikijenga mashambulizi kupitia kwa Shomari Kapombe ambaye alijitahidi kupanda kila mara wakati upande wa kushoto wa Stars haukuwa na mafanikio sana kwa sababu Oscar Joshua ni mzuri zaidi katika kuzuia na si mchezaji anayenyumbulika kirahisi, hivyo kazi ya kupanda na kurudi inakuwa ngumu kwake.

Baraka zile pia ziliendana na mawazo mapya aliyoyapata kocha kwa kuamua kumchezesha Ulimwengu katika nafasi sahihi anayotakiwa kucheza, huko nyuma niliwahi kushauri kwamba imefika wakati sasa wa Nooij kuamua kwa dhati nani anatakiwa aanze kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati ya John Boko au Thomas Ulimwengu ili mmojawapo aanzie benchi na pia mmoja kati ya Ngassa, Samatta, Msuva na Chanongo aanze kama mshambuliaji wa pili kuliko kulazimisha kuwachezesha wote wanne.

Kitu kizuri kimetokea juzi baada ya kocha kumchezesha Ulimwengu kama mshambuliaji wa kati kazi ambayo hupenda kuifanya kwa usahihi.

Haya ndio mafanikio mazuri anayoweza kuyapata kocha kwa kusikiliza ushauri mbalimbali hata kama unamkera sana.

Bila shaka tunahitaji kumpa muda Nooij ili wachezaji waendelee kuuzoea kwa faida ya timu yetu, lakini kama nilivyowahi kusema huko nyuma na naendelea kusisitiza Nooij lazima afuatilie kwa kina mengi kati ya maagizo yake anayoyatoa asiache yaelee kwenye karatasi yeye ni lazima awe zaidi ya kocha wa timu ya taifa.

Ushauri wa uchezaji kwa kuutumia mfumo huu ni lazima utumiwe na timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom na nyinginezo ili kumrahisishia kocha mkuu kazi ya utekelezaji.