Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ataiweza Man United inayojitafuta?

Amorin Pict
Amorin Pict

Muktasari:

  • Jina lake kamili ni Ruben Filipe Marques Amorim, ni mtoto wa mjini, alizaliwa Lisbon, Ureno mwaka 1985, kwa kiasi kikubwa alilelewa na mama  baada ya wazazi wake kuachana akiwa na umri mdogo sana. Alicheza nafasi ya beki wa kulia,  kiungo na winga.  Maisha yake ya soka yalianza katika timu za vijana za Clube Atletico Cultural mwaka 1998, kisha akatua Benfica na Belenenses.

LISBON, URENO: STORI kubwa ni kocha anayechukua mikoba ya kuinoa Manchester United, Ruben Amorim anayepewa asilimia nyingi za kufanikisha hilo na tayari mabosi wamekubali kuilipa Sporting Lisbon ya Ureno, kiasi cha Pauni 8 milioni ili kuvunja mkataba alionao. Aliwahi kuhusishwa na Liverpool na Manchester City.


AMORIM NI NANI?

Jina lake kamili ni Ruben Filipe Marques Amorim, ni mtoto wa mjini, alizaliwa Lisbon, Ureno mwaka 1985, kwa kiasi kikubwa alilelewa na mama  baada ya wazazi wake kuachana akiwa na umri mdogo sana. Alicheza nafasi ya beki wa kulia,  kiungo na winga.  Maisha yake ya soka yalianza katika timu za vijana za Clube Atletico Cultural mwaka 1998, kisha akatua Benfica na Belenenses.

Alipandishwa timu za wakubwa akianzia kucheza soka la kulipwa akiwa na Belenenses mwaka 2003 hadi 2008, kisha akatua Benfica, Braga na Al Wakrah kabla ya kustaafu.

Alistaafu mwaka 2017 akiwa na Benfica  na umri wa miaka 32, baada ya kupata jeraha kubwa la goti na akaambiwa kwamba itachukua muda sana kupona na kurudi tena uwanjani. Alibadilisha fani na kugeukia ukocha akivutiwa na  Jose Mourinho mmoja kati ya makocha anaowakubali. Alivutiwa na mbinu zake alizozionyesha akiwa na FC Porto, Chelsea, na Inter ambako alipata mafanikio sana. Mwaka 2018 alipata bahati ya kufundishwa masuala mbalimbali na Jose Mourinho kupitia semina ya High Performance Football Coaching. Baada ya hapo mwaka 2019 alipata kazi ya kuinoa  Braga, ambayo aliiwezesha kushinda taji la Portuguese Cup ikiwa ni baada ya nusu msimu tu.

Mafanikio yake akiwa na Braga yalisababisha vigogo wengine wa Ureno Lisbon, wavutiwe naye na ikafanikiwa kuipata huduma yake, misimu miwili ya kwanza akiwa na timu hiyo aliiwezesha kushinda taji la Ligi Kuu Ureno kwa mara ya kwanza baada ya miaka 19. Lakini mwenyewe hakubaliani na hili kwani anaamini Mourinho ni Mourinho yeye hawezi kufikia ukubwa wa kocha bora kama huyo.


Amorin 02
Amorin 02

UKWENI KUZURI

Armorim alifunga ndoa Mwaka 2013, na mrembo Maria Joao Diogo  kwenye kanisa la Palacio de S. Marcos church huko Coimbra, Ureno.

Kulikuwa na wageni 160 waliohudhuria sherehe hizo ikiwemo wachezaji na wadau mbalimbali wa soka duniani.

Wachezaji kama  Nuno Gomes, Miguel Vitor, Hugo Viana, Luis Filipe na Quim wote walikuwa sehemu ya sherehe hiyo. Alikuwepo pia kaka wa Maria aitwaye,  Antero Henrique.

Antero aliwahi kuwa mkurugenzi wa michezo wa PSG  na aliwahi kuhusishwa na Manchester United kabla mashetani hao wekundu hawajahamia kwa  Dan Ashworth.

Inaelezwa ukubwa na uzoefu wa shemeji yake huyo imechangia pia katika kumsimamia katika safari yake ya ukocha na kumwezesha kupata shavu la timu kama Braga na Sporting Lisbon.

Shemeji yake huyu ndio alisimamia pia dili la Neymar kutua PSG akitokea Barcelona lililogharimu zaidi ya Pauni 198 milioni.

Kabla ya kutua PSG aliwahi kufanya kazi yakuwa mkurugenzi wa mpira wa miguu wa FC Porto ambapo aliunda upya akademi yao na akaanzisha timu za mpira wa mkono na kikapu. Pia akasaidia kuanzishwa kwa makumbusho ya timu na chaneli ya televisheni.

Shemeji yake huyu ndio alihusika kumshawishi Kylian Mbappe akatae kujiunga na Real Madrid na atue PSG akitokea AS Monaco kwa wakati huo.

Kuna kipindi Dani Alves, alikuwa akihitajika na timu nyingi za Ligi Kuu England lakini yeye alimshawishi abaki PSG na ikawezekana. Shemeji mwingine wa Amorim ambaye ni dada yake Maria anaitwa Ines Diogo huyu ameolewa na mchezaji wa zamani wa Braga, Sporting Lisbon na Benfica, Luis Filipe.


KUTUPIA SIO POA

Kwenye masuala ya fasheni jamaa pia yupo. Anaonekana kabisa ataenda kupishana kwenye maduka ya nguo na makocha wengine kama Pep Guardiola, Mikel Arteta na Roberto De Zerbi ambao wanapenda mitindo.


Amorin 01
Amorin 01

ANASEMAJE KUHUSU UNITED?

“Manchester United inanihitaji, lakini ni chaguo langu kwenda au kutoenda, tusubiri hadi kila kitu kiamuliwe. Sina lolote la maana la kusema kwa sasa. Nitaendelea kufafanua kile ambacho nafanya siku zote, sitaki kuchochea suala hili. Kuna taarifa ya klabu imeshatolewa lakini siwezi kuongezea chochote,”alisema Amorim.

Hakuwapungia mkono mashabiki baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Nacional ambao unatajwa kuwa wa mwisho kabla ya kuondoka timu hiyo na alipoulizwa na waandishi wa habari alisema.

“Bado hakuna kilichoamuliwa, sijui kama ulikuwa ni mchezo wa kuwaaga au la.”

Alipoulizwa kuhusu hali ya wachezaji wake baada ya Sporting kutoa taarifa kwamba wamefikia makubaliano na Man United ambayo ipo tayari kuvunja mkataba wa kocha huyo, Amorim alisema ilikuwa ni ngumu sana kwake kuwatuliza wachezaji.

“Ni vigumu na ilikuwa karibu isiwezekane ni mpira wa miguu, kulikuwa na tangazo na lilitolewa siku ya mechi. Hilo haliko nje ya udhibiti wangu , kabla ya taarifa kutolewa, niliwaeleza wachezaji kila kitu kinachoendelea. Hali ya mashabiki na wachezaji haikuwa nzuri kiakili, lakini tulifanikiwa kufanya kazi yetu.’’


MASHABIKI WANAMLILIA

Katika mchezo dhidi ya Nacional mashabiki walidaiwa kuangusha machozi wakijua hiyo ndio itakuwa mechi ya mwisho ya kocha huyo. Taarifa kutoka Daily Mail imefichua kwamba mashabiki hawataki Amorim aondoke na wao wanaona itakuwa ni anguko lao.

Katika video moja iliyomuonyesha mzee mmoja akihojiwa na chombo cha habari huko Ureno, alipoulizwa kuhusu kuondoka kwa kocha huyo alijibu:”Itakuwa ni hasara kubwa kwetu,” kisha baada ya kusema maneno hayo aliangusha machozi.


MAFANIKIO

Ameshinda mataji sita, mawili ya Ligi Kuu Ureno ambayo yote alishinda akiwa na Lisbon kisha akashinda matatu ya  Portuguese League Cup ambapo moja alipata akiwa na Braga kisha mawili na Lisbon. Taji moja lililobakia ni lile la Portuguese Super Cup winner aliloshinda mwaka 2022 akiwa na Lisbon.


TIMU IPO?

Kutokana na kiwango ambacho Manchester United imekionyesha katika mchezo uliopita dhidi ya Leicester City baada ya kuondoka kwa Ten Hag  kimeonyesha kuwa bado timu hiyo ina wachezaji bora ambao wanaweza kumsaidia Amorim kutengeneza timu itakayokuwa tishio.

Wachezaji kama Casemiro ambao walikuwa wakihusishwa huenda wakauzwa kwa bei rahisi katika dirisha la majira ya kiangazi.

Van
Van

RUUD VAN  NISTELROOY VIPI?

Awali kumekwa na taarifa kwamba huenda kocha huyu akaondoka baada ya Amorim kuajiriwa kwani atakuja na benchi lake lakini ripoti zinaeleza watambakisha. Ruud ana uzoefu wa kutosha na United kama mchezaji na sasa kocha, anaaminika kuwepo kwake kutaleta mafanikio.