Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso kibaruani kuiba tiktak kutoka Catalunya kwenda Madrid

PAZIA Pict

Muktasari:

  • Xabi Alonso alizaliwa hapo Tolosa. Mikono yake ni misafi. Hana hatia ya siasa za Catalunya na Madrid. Majuzi nilikuwa Hispania na nilicheka nilipokuwa nasikiliza siasa za Catalunya na Madrid kwa mara nyingine.

TOLOSA, mji mdogo wenye manispaa katika Jimbo la Basque kule Kaskazini mwa Hispania. Ametoka kijana mmoja mwenye umri wa miaka 43 ambaye anapaswa kuifanya moja kati ya kazi ngumu pale Hispania.

Xabi Alonso alizaliwa hapo Tolosa. Mikono yake ni misafi. Hana hatia ya siasa za Catalunya na Madrid. Majuzi nilikuwa Hispania na nilicheka nilipokuwa nasikiliza siasa za Catalunya na Madrid kwa mara nyingine. Mtu wa Madrid hapaswi kwenda kufanya kazi Barcelona.

Mtu wa Barcelona pia hapaswi kufanya kazi Madrid. Nazungumzia katika mpira. Mapema wiki hii Alonso alitangazwa kuwa kocha wa Real Madrid. Hii nayo ni siri ambayo ilikuwa imefichwa vibaya. Kila mtu alikuwa anajua kwamba Alonso alikuwa anaelekea Madrid baada ya Carlo Ancelotti ‘kutimuliwa’ kwa busara.

Alonso ana kazi chafu, lakini lazima aifanye. Na kazi ya kuifanya Real Madrid iwe timu. Kwa sasa wana wachezaji tu ambao wana majina yanayotisha lakini timu hawana. Bahati nzuri Alonso ni aina ya makocha walewale wa Kihispaniola wanaofuata nyayo za kaka yao, Pep Guardiola.

Kuna Mikel Arteta anafanya kazi nzuri pale Arsenal. Kuna Cesc Fabregas anafanya kazi nzuri pale Como Italia na timu kubwa zinamtamani. Kuna Luis Enrique Martinez ambaye leo baadaye kidogo timu yake itacheza fainali za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya pale Munich.

PAZ 01

Mpira wao ndio mpira unaotamba zaidi duniani kwa sasa. Unaitwa Tiktak. ‘Nipe nikupe, halafu nikupe tena, halafu nipe tena’. Kazi kubwa ni kufungua nafasi na kupewa mpira. Na baada ya hapo kazi kubwa zaidi ni kukaba kwa haraka wakati hauna mpira.

Babu yetu Don Caro nadhani hakuuweza huu mpira katika dakika zake za mwisho za maisha ya Real Madrid. Haishangazi kuona namna Arsenal walivyoiteketeza Real Madrid kotekote. Walianzia Emirates hadi Santiago Bernabeu. Vipi kuhusu namna ambavyo Hans Flick anavyomteketeza Real Madrid kokote anakokutana naye.

Ndio maana Alonso yupo katika benchi la Real Madrid kwa sasa. Ana kazi ya kufanya ambavyo mpira wa kisasa unafanywa. Real Madrid hawakwenda kwa kocha mkongwe. Hawakumrudisha Jose Mourinho wala Antonio Conte. Walimtaka kocha ambaye atawapeleka mjini katika soka la Tiktak.

Alonso ana kazi ngumu kidogo. Kitu cha kwanza kabisa ni kuwashusha chini mastaa wake. Kwa sasa wanajiona wapo ghorofani. Hasa Kylian Mbappe na Vinicius Junior. Ni watu wa kutanua makwapa. Kucheza aina ya mpira wa Pep Guardiola inahitaji moyo.

PAZ 02

Ni kazi ya kitumwa hasa wakati hamna mpira. Akiwa na Bayer Leverkusen, Alonso alifanikiwa kwa sababu aliwaweka wachezaji wote chini ya nyayo zake. Kwanza yeye mwenyewe amecheza mpira kwa mafanikio kuliko wale wachezaji, lakini zaidi Bayer walikuwa hawajawahi kutwaa taji lolote la Bundesliga.

Sasa hivi amekwenda katika mikono ya kina Mbappe na Vinicius. Wana pesa. Wana majina makubwa. Wana uwezo wa kujiamini na mpira ukiwa mguuni. Hata hivyo, Alonso inabidi awashushe kwanza wajue kuwa timu ni muhimu kuliko wao. Pep aliwahi kukabiliwa na kazi hii.

PAZ 03

Alinusa alipofika katika kikosi cha kwanza cha Barcelona akaamua kuachana na Ronaldinho na Deco. Muda si mrefu Samuel Eto’o naye akafunga kabati lake na kwenda mji mkuu wa Italia, Milan. Pep akaifanya kazi yake vyema.

Arteta aliwahi kuifanya kazi hii. Alijua tu kwamba Mesut Ozil na Pierre Emerick Aubameyang wangemsumbua ndani na nje ya uwanja. Akaachana nao na kutengeneza timu ambayo msingi wake mkubwa ni namna inavyocheza kuliko kutegemea zaidi mastaa.

Alonso ataweza kuwaweka Mbappe na Vinicius mfukoni mwake? Hilo ni swali la kwanza. Kuwa nao katika timu ni faida kwa sababu wana uwezo mkubwa, lakini kitu cha kwanza ni namna ambavyo na wenyewe watakubali kuwa sehemu ya timu zaidi kuliko kuonyesha uwezo binafsi.

Wakati mwingine unaweza kukuta Alonso analazimika kumpanga mmoja tu kati ya Mbappe au Vinicus uwanjani kwa mujibu wa mfumo wake fulani au namna ambavyo anataka timu icheze.

PAZ 04

Hapo ndipo inapobidi awe na roho ngumu. Atalazimika kuwa na roho ngumu kwa wachezaji wenyewe, lakini atalazimika kuwa na roho ngumu kwa tajiri wa timu, Florentino Perez ambaye mara zote anapenda kuwaona mara zote wachezaji wake mastaa uwanjani kwa sababu za kibiashara.

Mpira upo mikononi mwa Alonso. Kitu ambacho tunataka kukiona ni namna ambavyo Alonso mwenye pesa atakavyotaka kama Vincent Kompany. Kule Bayer Leverkusen ilikuwa lazima Alonso afeli katika msimu wake wa pili. Timu ilikuwa imechoka baada ya mbio kali za kutwaa Bundesliga kwa mara ya kwanza. Na timu kama Bayer Leverkusen haina pesa za kununua wachezaji mastaa wa kuendeleza pale walipoishia. Lakini kwa Real Madrid Alonso ashindwe mwenyewe. Atachezea pesa kadri atakavyotaka.

Nimemsema na Kompany kwa sababu aliishusha daraja Burnley, lakini akaenda zake Bayern Munich na kutwaa taji la Bundesliga.

Bayern walijua kwamba alikuwa kocha mzuri, lakini asiye na pesa. Wakamuamini na sasa wamerudisha taji lao kutoka kwa Bayer Leverkusen. Na sasa Alonso ana kazi ya kuibadili Real Madrid. Ana kazi ya wizi ya kuhamisha mpira wa Catalunya kuupeleka Madrid.

PAZ 05

Na kama akifanikiwa basi hivi vipigo vya mbwa koko ambavyo Real Madrid inapokea kutoka kwa Barcelona kila kukicha huenda vikakoma. Akifanya kazi inayotakiwa sidhani kama itakuwa rahisi tena kwa Arsenal kuichapa Real Madrid pale London na chumbani kwake - Bernabeu.

Yale maisha yanaweza kutoweka. Lakini kuna kazi ngumu kwanza ya kufanya kwa sasa. Maisha hayatakuwa rahisi sana.