Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ally Mcharo; Kuokota mipira kulivyomvuta kucheza gofu

MCHARO Pict

Muktasari:

  • Katika mahojiano na Mwanaspoti, anasimulia safari yake ilianzia akiwa na umri wa miaka 10 siyo kwa kuc heza uwanjani bali kwa kuokota mipira iliyopigwa na wachezaji kisha ikapotelea katika vichaka na maji.

NYUMA ya mafanikio ya kila mtu, ipo stori ya kusisimua na kufunza wengine wanaojitafuta ili wasikate tamaa, kuamini kicheko chao kipo njiani, kama anavyosimulia mchezaji wa gofu wa ridhaa, Ally Mcharo kutoka klabu ya TPC, Moshi.

Katika mahojiano na Mwanaspoti, anasimulia safari yake ilianzia akiwa na umri wa miaka 10 siyo kwa kuc heza uwanjani bali kwa kuokota mipira iliyopigwa na wachezaji kisha ikapotelea katika vichaka na maji.

“Nyumbani kwetu nilikozaliwa tulikuwa karibu na viwanja vya gofu vya TPC Moshi,  hivyo mipira iliyokuwa inapotea wachezaji wakipiga tunaenda katika nyasi ndefu au kwenye maji tunaokota na kuwauzia,” anasema Mcharo na kuongeza;

MCHA 01

“Kuna wakati nilikuwa naokota mipira 20 kwa kipindi hicho mmoja nilikuwa nauza Sh1000, hivyo kupata Sh10,000 hadi 20,000 nikawa nashawishika kuupenda mchezo huo, hicho kikawa chanzo cha kuupenda na kujiamini utanipa maisha.”

Anasema amezaliwa katika familia ya watoto watano, ndugu zake Sanura, Seif, Juma na Nashe wote wanacheza gofu, sababu ikiwa ni moja tu iliyowaingiza katika mchezo huo ni ukaribu wa viwanja vya gofu na nyumbani kwa wazazi wao.

MCHA 02

“Pamoja na hilo wazazi wetu hawajawahi kuc heza gofu kabisa,” anasema. Mcharo siyo muumini mkubwa wa kuviweka vitu vyake hadharani alivyovipata kupitia gofu, ila ameshindwa kujizuia kuhusu elimu kusoma hadi ngazi ya degree katika chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) kitaaluma ni mwalimu hatua hiyo ya kielimu ilitokana na mchezo huo.

“Baada ya kumaliza darasa la saba nilianza kufanya kazi ya ukedi, nilikuwa nabeba mabegi ya mzungu mmoja alikuwa anaitwa John Sargent alifanya kazi ya umeneja hapo TPC kwa miaka 10, aliniambia napaswa kucheza gofu, nilimwambia changamoto ni vifaa, alininunulia vya gharama, lakini alitaka niwe nacheza naye huku nikiendelea kumbebea vifaa,” anasema na kuongeza;

MCHA 03

“Jambo la msingi alinisisitiza elimu na kuniambia lazima niwe na fani nyingine ya kuniingizia kipato, aliamini gofu pekee haiwezi kubadilisha maisha yangu, akijitolea mfano yeye mwenyewe ni mchezaji lakini ni meneja, baadaye akaondoka.

“Wengine ambao ni sababu ya mimi kufika chuo kwa kujitoa kipesa na ushauri ni Robert Baisaac na Jaffary Ally, walinisisitiza elimu itakayonipa fani ya kunisaidia maisha yangu.”

Mcharo aliye na handcup 2+ anasema kiwango hicho kinatokana na kupiga mipira chini ya 70 ambayo haizidi par 72 ya viwanja ambavyo ili viwe bora duniani kote lazima viwe na par 72.

MCHA 04

“Changamoto iliyoniweka nje, mchezaji unapokuwa kwenye piki ya juu kiuchezaji, lazima kuwepo na hatua nyingine zaidi mbele kama kutani kwenda uproo, nimeona wachezaji kama watano ambao waliandika barua ya kuomba kutani hawajajibiwa hadi sasa,” anasema na kuongeza; Pia maproo wanakosa mashindano ya muendelezo kwa sababu hakuna uhakika wa udhamini wa kufanya mashindano ya mara kwa mara, hiyo ikawa sababu ya mimi kutafuta kazi ambapo kwa sasa nafanya kazi kiwanda cha Tumbaku kilichopo Chunya nikiwa Agricultural Labour Practices, Technician, majukumu yangu makubwa hapo ni kuhakikisha hakuna utumikishwaji wa watoto, haki za wafanya kazi, kusimamia ukilima wa kisasa.”

MCHA 05

Miongoni mwa tuzo kubwa alizowahi kuzichukua ni PDF mwaka 2019, Lugalo Open, Arusha Open, Morogoro Open na amewahi kuwa Tanzania One namba mbili.