Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ali Daei, Ronaldo ndo kavunja rekodi yake kimataifa

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Daei aliyeifundisha timu hiyo kuanzia mwaka 2008 hadi 2010 alipotimuliwa baada ya Iran kushindwa kupata tiketi ya ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2010, alisema hawezi kulitumikia taifa lililosahau mchango wake na kumdhalilisha yeye na familia yake kwa muda mrefu.

KWA mara nyingine mchezaji nyota wa kandanda wa Iran, Ali Daei, aliyetamba miaka ya nyuma amekataa ombi la kuwa kocha wa timu ya taifa wa nchi hiyo.

Daei aliyeifundisha timu hiyo kuanzia mwaka 2008 hadi 2010 alipotimuliwa baada ya Iran kushindwa kupata tiketi ya ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2010, alisema hawezi kulitumikia taifa lililosahau mchango wake na kumdhalilisha yeye na familia yake kwa muda mrefu.

Alifungiwa biashara zake, akanyang’anywa hati ya kusafiria na familia yake kuwekewa vikwazo vya kusafiri kwa sababu aliilaumu serikali kwa kuzuia watu kutoa maoni juu ya mwenendo wa serikali yao.

Miaka minne iliyopita zilisikika habari za Daei kutaka kufunguliwa mashitaka ya uhaini ili auliwe, lakini vilichomoza vikundi vya vijana na mashabiki wa kandanda waliotaka kufanya vurugu nchi nzima kupinga njama hizo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Baada ya kuona hali ni tete, serikali ikarudi nyuma na kupunguza kumlaani Daei.

Mara nyingi Daei alisema alitishiwa kuuawa kwa vile aliwaunga mkono watu walioandamana kuipinga serikali ya Iran.

Daei aliyestaafu kucheza kandanda 2006 baada ya kuifungia timu ya taifa ya Irani mabao 109 katika mechi za kimataifa, aliwahi kuombwa awe Rais wa Shirikisho la Soka la Iran na kukataa na akisema sio vizuri kumpa mhaini jukumu la kuliongoza taifa katika michezo.

Serikali ya Iran ilidai alijipatia utajiri kwa njia haramu, lakini mtandao wa michezo wa Ujeruman Transfermarkt, ulisema Daei alipata zaidi ya dola milioni 16 za Kimarekani alipochezea klabu za Arminia Bielefeld na Bayern Munich vya Ujerumani, Al Shabab ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Al Sadd FC ya Qatar.

Baada ya kustaafu rafiki zake walimtaka abakie Ujerumani kufanya biashara, lakini alisema aliamua kuwekeza kwao Iran na kufungua kampuni ya biashara na hoteli zilizotoa ajira kwa vijana 15,000.

Kilichoiudhi serikali ya Iran ni kufungua mfuko wa kuwasaidia watu wa Kurdistan waliopata maafa ya tetemeko la ardhi kwa kuwanunulia chakula, nguo na dawa na kuwapa pesa walioathirika vibaya.

Hii ilitafsiriwa kama kujijenga kisiasa, lakini akasema hana hamu ya siasa, lakini hatakaa kimya serikali ikifanya dhulma na kutojali raia zake.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Miaka 20 iliyopita Daei alikuwa mchezaji wa kwanza duniani kufunga mabao 100 katika mechi za timu za taifa na rekodi hiyo ikadumu kwa miaka 15 kabla ya kuja kuvunjwa na Cristiano Ronaldo wa Ureno mwaka 2021.

Kwa bahati mbaya mara nyingi wanapozungumzwa wachezaji kandanda mahiri kwa kufunga mabao, jina la Ali Daei sio kawaida kusikika.

Mpaka hivi karibuni alipoibuka Cristiano Ronaldo, Daei alikuwa mchezaji aliyeongoza duniani kwa kufunga mabao mengi kwa nchi yake katika michezo ya kimataifa.

Daei alipendwa kwao Iran na kupachikwa jina la Mfalme Asiyekuwa na Maringo, mbwembwe au majivuno na siku zote anasema mamafanikio yake yametokana na msaada wa wachezaji wenzake.

Aliwahi kusema; “Ninawashangaa wanaonipa mimi heshima kwa rekodi yangu. Hii sio rekodi yangu binafsi bali ni ya watu wa Iran na hasa wachezaji wenzangu.”

Daei alizungumza na vyombo vya habari alipoivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mchezaji wa zamani wa Hungary, Ferenc Puskas aliyefunga mabao 84 katika mechi 85 katika miaka ya 1950.

Rekodi ya Puskas ilidumu kwa miaka 40. Wengi wanaamini rekodi ya Daei ingekuwa nzuri zaidi na tabu kufikiwa kama asingelazimika kuacha kandanda kwa muda ili kuitumikia nchi yake jeshini.

Urefu wake wa futi 6 na inchi 4 uliwapa tabu wachezaji wa upinzani wakati mpira ukiwa hewani, hasa ilipopigwa kona.

Kila ulipopigwa mpira wa kona, macho ya watazamaji yalimuangalia Daei, lakini jingine lililowavutia ni alivyoumiliki mpira mguuni na kwenda nao kwa kasi kama vile miguu yake ilikuwa na smaku.

Aligombaniwa na klabu nyingi na ya kwanza kumchukua ilikuwa Al-Sadd ya Qatar na baaadaye alikwenda Ujerumani kujiunga na Arminia Bielefeld pamoja mchezaji mwenzake wa Iran, Karim Bagheri.

Wachezahi hawa wawili ndio waliofanya mauaji maarufu ya 17-0 pale Iran ilipochea na Maldives katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia.

Alipostaafu alichaguliwa kocha wa Iran, lakini mambo hayakumwendea vizuri kama alivyokuwa mchezaji na hii  ilitokana na kuingiliwa na viongozi wa kandanda na serikali katika kupanga wachezaji.

Hivi sasa Daei ambaye ana umri wa miaka 55, ni mfanyabiashara kwao Iran na nchi za jirani, hasa wa vifaa na mavazi ya michezo.

Alichaguliwa Balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto (UNICEF) mwaka 2001 na mjumbe wa Kamati ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kuanzia mwaka 2007 hadi 2013.

Mwaka 2014 jina lake liliingizwa katika ukumbi wa Wachezaji Maarufu wa Asia.

Daei ambaye ni msomi wa uhandisi katika Chuo Kikuu cha teknolojia cha Seriff kiliopo Iran, alianza safari ya mafanikio katika soka kwa kujiunga na klabu ya Esteghlal ya mji wa Ardabil alikozaliwa.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Baadaye alijiunga na Taxirani FC ya Tehran aliyoichezea kwa miaka saba kabla ya kujiunga na klabu ya Bank Tejarat FC aliyokaa nayo kwa miaka minne na kuifungia mabao 49 katika mechi 75.

Daei alikuwa mchezaji wa kwanza wa Asia kucheza katika mashindano Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Mei 28, 2007 Daei alitangaza kustaafu kucheza na kuwa mwalimu kwa kuanzia na klabu ya Saipa ya Iran na kuiwezesha kuwa klabu bingwa ya Ghuba ya Persia na baada ya hapo akachaguliwa kocha wa timu ya Iran.

Baada ya kutimuliwa kuwa kocha wa Iran mwaka 2009 aliifundisha klabu ya Persepolis na baadaye klabu ya Rah Ahan na kufanya maguezi kwa kuwachukua vijana kushika nafasi za wakongwe.

Aliisogeza timu hiyo kutoka kumaliza katika nafasi ya 13 katika ligi na kuwa ya 11 na msimu wa 2012 ilimalizia nafasi ya nane, nafasi ambayo mara ya mwisho timu hiyo kuifikia ilikuwa mwaka 1937.

Aliacha baada ya kuanza vibaya katika ligi na kuifundisha Saba Qom kwa mkataba wa miaka miwili na baada ya kila muda mfupi alifundisha klabu nyingine.

Alipoulizwa kwa nini alibadili klabu baada ya kila muda mfupi alijibu: “Nilipokuwa ninacheza nilikuwa situlii na kukaa sehemu moja kama basi lilioegeshwa kungojea abiria. Sikusubiri kuletewa mpira, nilihangaika kuutafuta na hivyo hivyo ndivyo nilivyo kama mwalimu wa soka.”