Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zulay na Paul Pogba katika milima na mabonde

Muktasari:

  • Kwa miaka zaidi ya saba, uhusiano wa Pogba, 32, na Maria, 32, umegusa hisia za mashabiki wengi huku ukichukuliwa kama mfano bora wa upendo wa kweli, ustahimilivu na mshikamano usio na mwisho.

Dunia inamfahamu Paul Pogba kama mchezaji maarufu wa soka aliyecheza katika klabu kubwa ikiwemo Manchester United na Juventus, pia maisha yake binafsi hasa ndoa yake na Maria Zulay, imepelekea mashabiki wengi kupenda kumfuatilia.

Kwa miaka zaidi ya saba, uhusiano wa Pogba, 32, na Maria, 32, umegusa hisia za mashabiki wengi huku ukichukuliwa kama mfano bora wa upendo wa kweli, ustahimilivu na mshikamano usio na mwisho.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2017, wakati Pogba alipokuwa jijini Los Angeles, Marekani kwa ajili ya mashindano ya International Champions Cup ambayo Man United ilishiriki.

Kipindi hicho Zulay alikuwa akifanya kazi ya uanamitindo mjini Miami, na punde tu akaanza kuonekana mara kwa mara kwenye mechi za Pogba huko Uingereza kitu ambacho kilimfanya kuipa kisogo kazi yake mitindo.

Tetesi za uhusiano wao na hata kuchumbiana zilishika kasi pindi Zulay alipoonekana amevaa pete wakati apohudhuria mechi za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi akiwa ameongoza na mama mzazi wa Pogba.

SHO 01

Mei 2019, mrembo huyo alibadili jina lake katika mtandao wa Instagram na kuanza kutumia 'Zulay Pogba' akiwa amechukua jina la familia ya mchezaji huyo, hilo lilibua hisia huwenda wawili hao wamefunga ndoa kimya kimya.

Hatua hiyo ilikuja wiki moja baada ya wawili hao kuhudhuria tuzo za mchezaji bora wa msimu wa Man United ambapo katika hafla hiyo Pogba alionekana akiwa amevaa pete kidoleni na ndipo zikaibuka tetesi huwenda wamefunga ndoa.

"Mimi na wewe hadi milele," ni ujumbe alioundika Zulay Instagram walipokuwa wakifurahia mapumziko pamoja huko Paris, Ufaransa, na haikuchukua muda ikathibitika ni kweli Pogba na Zulay wameoana rasmi.

Ndoa hiyo ilikuja miezi michache baada ya hapo Januari 3, 2019 kujaliwa mtoto wao kwanza, Labile Shakur ambaye alikuwa akionekana mara kwa mara katika uwanja wa Old Trafford akimuunga mkono Pogba.

SHO 02

Pogba alisherehekea kuzaliwa kwa mtoto huyo alipofunga penalti dhidi ya Brighton katika mchezo wa Ligi Kuu England (EPL) ambapo alishangilia kwa mtindo wa kubembeza mtoto.

Tangu wakati huo, Zulay amekuwa kando yake katika nyakati zote za maisha, amesafiri naye duniani na kuhudhuria matukio makubwa, ikiwemo Kombe la Dunia 2018 ambapo Pogba aliisaidia Ufaransa kutwaa ubingwa mbele ya Croatia.

Licha ya kuishi maisha ya faragha, uhusiano na Pogba ulimfanya Zulay kupata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kupitia mtindo wake wa kisasa wa maisha.

Kwa sasa familia ikiwa imeongezeka wakiwa na watoto watatu, wenzi hao wamechagua kuweka maisha ya familia yao faragha, ni mara chache sana hutoa taarifa kuhusu watoto wao, mathalani mtoto wao mwisho aliyezaliwa Mei 2023, bado jina lake hawajaliweka wazi.

SHO 03

Hata hivyo, haimaanishi kuwa wanaificha sana familia yao, hapana!, kuna nyakati Zulay au Pogba huweka picha na video za kupendeza mtandaoni akiwa na wanawe maeneno mbalimbali kama uwanjani, ufukweni, hotelini n.k.

Akiwa kama wanasoka mahiri aliyeshinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A), kazi yake imekumbwa na misukosuko mingi, mmoja wapo ni kufungiwa baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli kinyume na sheria za michezo. 

Pogba ambaye mara ya mwisho kuiichezea timu yake ya taifa ilikuwa Machi 2022, alifungia miaka minne lakini baada ya kukutaa rufaa adhabu ilipunguzwa hadi miezi 18, na kufikia Machi 2025 akarejea uwanjani akisajiliwa na AS Monaco.

SHO 04

Akiwa anatumia adhabu hiyo ambayo ilipelekea Juventus kuvunja mkataba wake, mchezaji huyo wa Ufaransa alitumia muda wake na familia yake. Alipata muda wa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mkewe, jambo ambalo lilimfurahisha sana Zulay hadi kwenda Instagram kushukuru.

"Karibu mwaka wangu wa 31!. Najihisi mwenye shukrani na kubarikiwa kwa kila mtu na kila kitu. Asante sana mpenzi wangu kwa kufanya haya yote kutimia," alieleza Zulay ambaye alibadili dini baada ya kuolewa na Pogba.

Julai mwaka huu, Pogba baada ya kusaini AS Monaco, katika mahojiano ya kipekee alifichua mengi na hata kububujikwa na machozi akisema kwamba wakati wa nyakati ngumu za kuwa nje ya soka, mkewe alimsaidia sana kuwa sawa.

"Siwezi kushukuru vya kutosha kwa kila kitu nilichonacho," aliandika Zulay katika siku yake ya kuzaliwa alipotimiza miaka 30, kisha akaendelea akitoa ujumbe kwa Pogba.

SHO 05

"Wakati mwingine mambo hayaendi kama tunavyotaka na huwezi kubadilisha chochote, lakini unaweza kufurahia na kuthamini kila wakati ukiwa na watu unaowapenda, wanaokufanya uwe na furaha na kukufanya uwe mtu bora kila siku," alieleza.

Ikumbukwe Zulay alizaliwa Novemba 16, 1993 huko Robore nchini Bolivia, wazazi wake ni Ricardo na Karla. Yeye ni wa tatu akiwa na dada zake wawili, Caria na Gabriela. Alisomea usimamizi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Bolivia na baadaye akahamia upande wa mitindo, kisha usanifu wa mambo ya ndani.