Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 20 baada ya Mr. Blue kutamba na Mapoz

Muktasari:

  • Msanii huyo amefanikiwa kuachia kazi nyingi ambazo zimefanya vizuri lakini nyimbo zake mbili za mwanzo ndizo hasa zimebeba historia yake kwa sehemu kubwa. Fahamu zaidi.

KATI ya wasanii ambao wameishi umaarufu kwa miaka mingi, Mr Blue ni mmojawao kwani nyimbo zake zilianza kufanya vizuri akiwa bado kijana mdogo aliyetambua kipaji chake mapema.

Msanii huyo amefanikiwa kuachia kazi nyingi ambazo zimefanya vizuri lakini nyimbo zake mbili za mwanzo ndizo hasa zimebeba historia yake kwa sehemu kubwa. Fahamu zaidi.


1. Mr Blue alianza muziki chini kwa Dudu Baya Foundation akiwa na wenzake wengi aki wemo Nyandu Tozzy, zamani Dogo Hamidu ambaye baadaye sana walikuja kufanya kazi pamoja katika kundi la B.O.B Micharazo.


2. Dudu Baya alipenda rapa huyo atunge nyimbo za kuelimisha jamii zaidi lakini Mr. Blue alipendelea nyimbo za kishua na za kula bata zaidi, kitu kilichofanya akose nafasi ya kurelodi chini ya taasisi hiyo. Wakati huo tayari Dudu Baya alishavuma kupitia ngoma yake, Mwanangu Huna Nidhamu (2000) iliyorekodiwa Sound Crafters kwa Enrico Figueiro ila mdundo ulitengenezwa MJ Records na Master J.

3. Akiwa Club Asset pande za Kinondoni, Dar es Salaam, Mr Blue akakutana na mtayarishaji muziki Roy na kumuomba ampatie nafasi ya kurelodi baada ya kuona kwa Dudu Baya kuna ufinyu wa nafasi.


4. Basi Roy akamkaribisha Mr Blue katika studio za G Records, na alimtengenezea wimbo uliomtoa kimuziki na kumpa heshima kubwa, Blue Blue (2003) uliobeba jina la albamu yake ya kwanza.


5. Blue Blue ni kati ya nyimbo ambazo Dudu Baya alizikataa akisema zinalenga kuhamasisha starehe wakati jamii inahitaji muziki wa kuelimisha. Mbali na Blue Blue, pia aliukataa wimbo mwingine wa rapa huyo uitwao Bonge la Gari. Hata hivyo, kabla ya kurekodi Blue Blue, Mr Blue alikuwa amesharekodi wimbo mwingine uitwao ‘Yatima’ lakini haukufanikiwa kumtangaza, hivyo kwa ujumla Blue Blue ilikuwa wimbo wake wa pili kurekodi.

6. Kipindi Blue Blue inatoka, Mr Blue alikuwa na umri wa miaka 15, umaarufu mkubwa alioupata kipindi wimbo huo unatoka ulimfanya kuacha shule wakati huo akiwa kidato cha kwanza. Huo ni wimbo uliopelekea kubadili jina lake katika muziki kutoka Lil Sameer na kuwa Mr Blue, mwanamuziki aliyetamba na ngoma yake, Pesa (2014).


7. Roy haikuishia kwa Blue Blue, bali alitengeneza wimbo mwingine uliompa heshima kubwa Mr Blue, Mapozi (2003) ambao uliongeza umaarufu wake na kumpatia show nyingi za ndani na nchi jirani kama Kenya.


8. Miaka 20 baadaye, Diamond Platnumz alikuja kuurudia wimbo Mapozi, na kuja na wake, Mapoz (2023) ambao alishirikiana na Mr Blue pamoja na Jay Melody, staa aliyetoka na ngoma yake, Goroka (2018). Hadi sasa hiyo ndio ngoma ya Mr Blue ambayo imefanya vizuri zaidi YouTube ikitazamwa zaidi ya mara milioni 37.3.


9. Video ya Mapoz ikiongozwa na Director Ivan, ilinogeshwa na mwigizaji Nana Dollz ambaye awali alitokea kwenye video za wasanii kama Aslay (Natamba 2017) na Alikiba (Utu 2022).

10. Mapoz ni wimbo wa tatu kwa Mr Blue na Diamond kushirikiana, hapo awali alishatoa nyimbo kama Nakupa Moyo Wangu (2010) kutoka katika albamu ya kwanza yake Diamond na BBM (2013) wake Ngwea.