Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema amaliza utata pesa za Idris

Muktasari:

  • Idris alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wema kati ya mwaka 2015-2016 ikiwa ni miezi michache tangu alivuna Sh 500 kutokana na ushindi wa BBA na mara baada ya kuishiwa kwa fedha hizo, tuhuma zimekuwa zikielekezwa kwa mrembo huyo kwamba ndiye aliyezitumbua fedha.

MSHINDI wa shindano la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amemaliza utata juu ya madai ya kumfilisi fedha za ushindi wa Big Brother Afrika 9: 'Hot Shots', aliyekuwa mpenzi wake Idris Sultan baada ya kushinda shindano hilo kwa mwaka 2024.

Idris alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wema kati ya mwaka 2015-2016 ikiwa ni miezi michache tangu alivuna Sh 500 kutokana na ushindi wa BBA na mara baada ya kuishiwa kwa fedha hizo, tuhuma zimekuwa zikielekezwa kwa mrembo huyo kwamba ndiye aliyezitumbua fedha.

Hata hivyo, juzi Wema aliamua kumaliza utata kwa kuweka bayana juu ya tuhuma huizo kwa kusema;

“Ngoja leo nikwambie kitu ambacho Watanzanzia wengi hawakijui, ila wananipa tu shutuma zinazoniumiza sana kila kukicha, mimi, sikuwahi kuchukua hata shilingi moja kutoka kwa Idris, hata yeye analijua hili na  anajua jinsi alivyopoteza pesa zake. Sihusiki na tuhuma hizo."

Wema, alisema anatamani siku moja Idris ajitokezea na kulizungumzia suala hilo ili kuepuka watu kuendelea kumshtumu ila anamshangaa kwa kuamua kukaa kimya hadi leo wakati anajua ukweli ulivyo.

“Anachotakiwa Idris ni kujitokeza hadharani kusema ukweli kama mimi sihusiki na pesa zile za Big Brother,  hili ingekuwa ni jambo la busara sana," alisema Wema aliyeamua kujitosa katika fani ya filamu mara baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania 2006.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilipomuuliza Idris kuhusu kauli hii ya Wema, mchekeshaji na mwigizaji huyo wa filamu alisema hawezi kuzungumzia jambo lililopita, ikizingatiwa kwa sasa hawapo pamoja tena na Wema zaidi ya kupiga kazi tu.