Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wageni waanza kutua Zenji kuwahi tamasha Sauti za Busara

Muktasari:

  • Tamasha hilo lenye kauli mbiu 'Voices For Peace' (Sauti za Amani), ni kati ya matamasha makubwa duniani yanayokutanisha wasanii na watalii kutoka nchi mbalimbali kwa pamoja na kutumbuiza nyimbo tofauti zikiwamo za utamaduni.

WAGENI kutoka nchi mbalimbali wameanza kumiminika visiwani Zanzibar kuhudhuria Tamasha la Kimataifa za Sanaa la Sauti za Busara litakaloanza Februari 14 hadi 16 kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe, Unguja.

Tamasha hilo lenye kauli mbiu 'Voices For Peace' (Sauti za Amani), ni kati ya matamasha makubwa duniani yanayokutanisha wasanii na watalii kutoka nchi mbalimbali kwa pamoja na kutumbuiza nyimbo tofauti zikiwamo za utamaduni.

Akizungumza na Mwanaspoti, mratibu wa tamasha hilo, Journey Ramadhan amesema imebaki wiki moja tu kuanza kwa tamasha na wameanza kupokea wadau kutoka sehemu tofauti.

"Tamasha letu mwaka huu lina mwamko mkubwa, tumeanza kupokea wadau kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanakuja kwa ajili ya kushuhudia msimu huu wa 22," amesema Ramadhan na kuongeza;

"Wasanii watakaotoa burudani wanatarajia kufanya kongamano ambalo litafanyika kwa siku mbili, tutazungumzia changamoto za muziki, kipi kifanyike ili kuwasaidia wasanii, na mwaka huu tutafunga majukwaa manne ambayo yataanzia Ngome Kongwe, Forodhani na Fumba na kongamano hilo ni la masuala ya muziki kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wasanii."

Baadhi ya wanamuziki wanaotarajiwa kuwasha moto katika tamasha hilo kutoka Tanzania ni Christian Bella & Malaika Band, Frida Amani, Zanzibar Taarab Heritage Ensemble, Leo Mkanyia & Swahili Blues, Tryphon Evarist, Baba Kash na wengine wengi.

Pia wapo wakali kutoka nje ya nchi kama Thandiswa (Afrika Kusini), Blinky Bill (Kenya), Bokani Dyer (Afrika Kusini), The Zawose Queens (TZ/UK), Kasiva Mutua (Kenya), Boukouru (Rwanda), Charles Obina (Uganda), Assa Matusse (Msumbiji), Mumba Yachi (Congo), Nidhal Yahyaoui (Tunisia), Etinsel Maloya (Reunion), WD Abo (Sudan), B.Junior (Mayotte), uKhoiKhoi (Afrika Kusini), Joyce Babatunde (Kamerun) na wengineo.

Tamasha la Sauti za Busara lilianzishwa mwaka 2003 na hufanyika kila mwaka ndani ya Februari katika Mji Mkongwe, Zanzibar na mwaka huu ni msimu wa 22.

Tamasha hili linaangazia muziki wa Kiafrika, likiwa na lengo la kuenzi na kuendeleza muziki wa asili kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika na kwa miaka mingi, tamasha hili limekuwa jukwaa muhimu kwa wasanii wa Kiafrika kuonyesha vipaji vyao na pia kuvutia wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia.