Kisa pete Kajala awekewa ulinzi mkali

Muktasari:
- Mwanaspoti limetonywa, Kajala amewekewa ulinzi huo na mumewe huyo mtarajiwa ambaye amekuwa akifichwa jina lake huku akipigwa biti kuachana na kiki zinazohusu mapenzi kwani zinamshushia hadhi hiyo jamaa yake.
KAMA uliwahi kumkatia tamaa msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja kwa kudai umri umeenda na hatoweza kuolewa, basi imekula kwako, kwani tayari ameshavalishwa pete ya uchumba na kuwekewa ulinzi mkali kila aendapo.
Mwanaspoti limetonywa, Kajala amewekewa ulinzi huo na mumewe huyo mtarajiwa ambaye amekuwa akifichwa jina lake huku akipigwa biti kuachana na kiki zinazohusu mapenzi kwani zinamshushia hadhi hiyo jamaa yake.
“Habari ya sasa mjini ni Kajala amepata Pedeshee na tayari ameshavishwa pete ya uchumba na baada ya kuvalishwa amewekewa ulinzi binafsi, hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.”
Mwanaspoti lilimtafuta Kajala ili kuthibitisha habari njema hizi na alisema maneno machache tu, wakati wa Mungu ni sahihi na kufanya mambo kimya kimya ni vema zaidi kwake.
“Waoooh hizi habari unazonipa ni jambo la kheri kwangu, lakini niseme tu kwa sasa mambo yangu ya mahusiano siwezi kuyaweka wazi basi kama suala hilo lipo basi vyema zaidi kwangu “Kuhusu kuonekana na pete mkononi ni jambo la kawaida kwa mwanamke na hata ishi ya kuwa na walinzi sehemu tofauti tofauti napokuwa pia ni kawaida na ni kwa ajili ya usalama zaidi” alisema Kajala.