Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya penzi haijawaacha salama

MAPENZI Pict

Muktasari:

  • Mwanaspoti linakuletea baadhi ya mastaa wa Bongo ambao wameingia kwenye vita ya penzi baada ya kuchukuliana wapenzi wao. Ni wazi kama mmeachana na ulikuwa bado unampenda au mmewahi kupata watoto, ukiona mtu anamchukua kimapenzi, lazima kuna maumivu fulani utayapata.

HII iko hivi, Kwenye ulimwengu wa mastaa hapakosekani vitimbi na mikasa ya hapa na pale, pia kwa watu wa kawaida huwa yanatokea mambo mengi, ila mastaa wanaonekana zaidi kwa kuwa wao ni kioo cha jamii na wengi wanawafuatilia maisha yao.

Mwanaspoti linakuletea baadhi ya mastaa wa Bongo ambao wameingia kwenye vita ya penzi baada ya kuchukuliana wapenzi wao. Ni wazi kama mmeachana na ulikuwa bado unampenda au mmewahi kupata watoto, ukiona mtu anamchukua kimapenzi, lazima kuna maumivu fulani utayapata.

Hii imewakuta baadhi ya mastaa na kujikuta wakiingia kwenye ugomvi na bifu kubwa huku wengine wakigeuka maadui wakati awali walikuwa marafiki wazuri.

MAPE 01

WEMA NA TUNDA

Wema Sepetu na video Vixen Tunda waliingia kwenye bifu baada ya Wema kumchukulia Tunda aliyekuwa mpenzi wake Whozu.

Kabla hayajatokea hayo, Wema na Tunda walikuwa marafiki na hadi waliwaita Tunda na Whozu kwenye kipindi chake cha mapishi kwa ajili ya 'interview', baada ya hapo Whozu na Wema wakaanza kuonekana ni wapenzi.

Baada ya Wema kumchukua mpenzi huyo wa Tunda hadi leo wawili hawa ni kama paka na panya kwani hawaelewani hata kidogo na  Whozu yuko na Wema hadi sasa.


MAPE 02

RUBY NA AUNT EZEKIEL

Mwimbaji nyota wa Bongo Fleva, Ruby na msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ni mahasimu walioingia kwenye mgogoro mzito wa penzi.

Wasanii hawa hadi sasa hawapendani baada ya Aunt Ezekiel kumchukua aliyekuwa mpenzi wa Ruby, Kusah ambaye ni msanii wa Bongo Fleva.

Awali Ruby alikuwa anaishi nyumba moja na Kusah na walipata mtoto mmoja, lakini baadaye waliweka wazi wameachana na Kusah kuhamia kwa Aunt. Hata hivyo, baadaye Ruby alidai chanzo cha kugombana na Kusah ni Aunt.

Aunt na Ruby kwa pamoja wamebarikiwa kupata mtoto na Kusah na Aunt ana watoto wawili na kusah na hadi sasa wanaishi pamoja.

MAPE 03

CHUCHU HANS NA JOHARI

Chuchu Hans na msanii mwenzake wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ ni mahasimu kwani hawapendani na chanzo kikidaiwa ni penzi la Ray.

Awali ilikuwa inadaiwa Ray na Johari ni wapenzi hadi wakafungua kampuni moja iliyojulikana kwa jina la RJ, licha ya kwamba hawajawahi kuanika hadharani penzi lao.

Penzi lao lilidaiwa kuvunjika baada ya Chuchu Hans kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray na wamejaliwa kupata mtoto mmoja na wanaishi pamoja.

Johari na Chuchu hadi sasa hawapendani na hawachangamani kabisa.

MAPE 04

RAYVANNY NA MARIOO

Wasanii hawa wa Bongo Fleva, waliingia kwenye vita nzito ya maneno baada ya kuchukuliana mwanamke Paula.

Rayvanny alikuwa anatoka kimapenzi na Paula na penzi hilo waliliweka wazi, ila baadae waliachana na ndipo Marioo akawa na Paula hadi sasa wanaishi pamoja na wamepata mtoto mmoja.

Marioo na Rayvvan walikuwa marafiki kabla ya tukio hili, ila walikuja kutupiana maneno ya mafumbo mtandao wa kijamii wa Instagram kuhusu Paula na hawaelewani kama zamani.

MAPE 05

DIAMOND NA DIMPOZ

Diamond aliingia kwenye vita ya penzi na Ommy Dimpoz baada ya Dimpoz kudai ametoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu. Hata hivyo, kwa wakati huo, Diamond na Wema walikuwa wametengana, lakini ilionekana bado alikuwa akimpenda na hivyo kuzua vita iliyochukua muda mrefu kwani Diamond alikasirika zaidi na urafiki wao ukaishia hapo.

Lakini miaka ya hivi karibuni wawili hao hasira zao zimeisha na sasa wanaelewana na baadhi ya sehemu za starehe mara nyingi wanakuwa pamoja.