Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shakira atambulisha mpenzi mpya!

Muktasari:

  • Msanii huyo mwenye umri wa miaka 49 aliyepewa tena jukumu la kutengeneza wimbo rasmi wa fainali za Kombe la Dunia baada ya mafanikio ya wimbo wake Waka Waka (This Time for Africa) uliotumika katika Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, bado anatrendi kwenye habari za soka kwa sasa ikizingatiwa kwamba wimbo wake ndi huo unawaka kwa sana.

MEXICO CITY, Mexico:KAMA bado unalitafakari biti kali la Dai Dai aliloliachia mwimbaji maarufu kutoka Colombia, Shakira Isabel, taarifa ikufikie kwamba ametambulisha mpenzi mpya anayetofautiana naye umri kwa miaka 15, mwigizaji wa filamu Lucien Laviscount.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 49 aliyepewa tena jukumu la kutengeneza wimbo rasmi wa fainali za Kombe la Dunia baada ya mafanikio ya wimbo wake Waka Waka (This Time for Africa) uliotumika katika Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, bado anatrendi kwenye habari za soka kwa sasa ikizingatiwa kwamba wimbo wake ndi huo unawaka kwa sana.

Shakira amezua mjadala kutokana na uhusiano wake huo na kijana huyo mwenye umri wa miaka 34, ambapo wawili hao walikutana wakati wa kurekodi video ya muziki ya Shakira 2024 ya Puntería, na muda mfupi baadaye uvumi ukaanza kuenea kuwa walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi, lakini walimudu kutoweka hadharani hadi wakati huu.

Laviscount, anayejulikana kwa majukumu yake katika kipindi cha televisheni Waterloo Road na mfululizo maarufu wa Netflix Emily in Paris, alionekana akila chakula cha jioni na Shakira katika jiji la New York na baadaye walionekana pamoja hadharani mara kadhaa. Hata hivyo mara zote walipoonekana pamoja iliezwa kwamba alikuwa akifanya kazi maalumu kama msaidizi wa mwanamuziki huyo katika mambo ya utawala.

Katika mahojiano na The Times, Shakira alisema: "Kwa sasa sina nafasi ya mahusiano ya kimapenzi. Sina muda wala nafasi katika maisha yangu kwa hilo. Nina majukumu mengi. Watoto wangu ni kipaumbele changu, pamoja na kazi yangu. Cha kushangaza ninaipenda kazi yangu kuliko wakati mwingine wowote katika maisha yangu. Pia ninafurahia muda wangu nikiwa peke yangu."

Iwapo uhusiano huo utaendelea kutrendi, basi Shakira atakuwa anapenda uhusiano wa kimapenzi na 'wadogo zake', kwani kwa miaka 12 alikuwa na Gerard Pique, staa wa zamani wa Manchester United na Barcelona ambaye anamuziki miaka 10. Hata hivyo, wawili hao waliokutana katika fainali za Kombe la Dunia 2010 huko Sauzi, waliachana 2022 baada ya kupata watoto wawili, Milan na Sasha.