Vikundi nane vyalamba Sh187 milioni za 'Feel Free

Vikundi nane vimeibuka kidedea na kulamba za mawazo ya kibunifu kupitia mradi wa Feel Free, zilizoandaliwa Nafasi Art Space.

Akitangaza vikundi hivyo vilivyoshinda Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Bodi Nafasi Art Space, Paul Ndunguru, alivitaja vikundi hivyo kuwa Fahari Yetu kutoka Iringa, Adea Tanzania kutoka Mtwara, Victoria Alex John kutoka Tanga, Wifi women prints kutoka Zanzibar.

Vikundi vingine ni Emedo kutoka Mwanza na Refixit kutoka Dar es Salaam, Scolastica Sultan na mradi wa ndoto ya Kalista na bendi ya muziki ya Bahati wote hawa wakitoka Dar es Salaam.

Ndunguru amesema vikundi hivyo vimeshinda ikiwa tatu toka program hiyo imeanza ambapo walioshinda ni wale walioandika wazo la kibunifu la upekee.

Amesema programu iliyopo chini ya ufadhili wa ubalozi wa Uswisi na Norway iliandaliwa kwa lengo la kuwatia moyo wasanii, wadau wa Sanaa, taasisi zinazojihusisha na ubunifu na sanaa ambao alitakiwa kupeleka wazo la kibunifu wanaloweza kufanyika kazi kisha kupewa  fedha za kuendesha miradi husika kwa uhuru.

"Wakati tunaendesha programu hii, zaidi ya watu na vikundi 100 vilijitokeza kuleta mawazo yao, lakini hivi vinane ndivyo vilishinda na sasa vitakwenda kutekeleza kile walichokiomba katika miradi yao,"amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha ametumia nafsi hiyo kuwashauri  wasanii waendelee kuzifuatilia programu zao ili wanufaike.

Kwa upande wao washindi akiwemo  Scolastica Sultan amrsema mradi wake umelenga kuwasaidia wanawake wanaolea watoto bila ya baba (Single mother) kuwaelimisha namna ya kuinuka baada ya kubaini wapo waliopoteza mwelekeo baada ya kupata ujauzito wakiwa wadogo.

Naye Aliabu Sadock kutoka taasisi ya Fahari Iringa amesema wao watakusanya taarifa za masimulizi yaliyopita ya kikoloni kutoka mkoani humo na kuyarudisha kwa jamii kwa ajili ya kujifunza maadili.