Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utata ndoa ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto

HAMISA Pict

Muktasari:

  • Ukaribu wa Aziz na Hamisa umekuwa ukizua maswali mengi katika mitandao ya kijamii, wengi wakidai wawili hao wanaigiza tu kwamba sio wapenzi, huku pia uvumi mwingine ukidai Aziz yuko karibu na kimwana huyo kama 'kava' tu ya kumlindia siri tajiri, ambaye amehusishwa kuwa ndiye mpenzi halisi wa Hamisa.

Wakati habari zimezagaa kila kona ya jiji kuwa mwanamitindo Hamisa Mobetto anaolewa Februari 15, 2025 na mchezaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki, mama wa mwanamitindo huyo ameongea jambo zito linalochochea utata kuhusu ndoa hiyo.

Ukaribu wa Aziz na Hamisa umekuwa ukizua maswali mengi katika mitandao ya kijamii, wengi wakidai wawili hao wanaigiza tu kwamba sio wapenzi, huku pia uvumi mwingine ukidai Aziz yuko karibu na kimwana huyo kama 'kava' tu ya kumlindia siri tajiri, ambaye amehusishwa kuwa ndiye mpenzi halisi wa Hamisa.

Ndio maana hata tangazo kwamba wawili hao wanatarajia kuoana lilipotolewa leo, limeendelea kuwaweka njia panda mashabiki ambao wengine wamebaki kuwa wazito kuamini kama kweli kuna ndoa ama ni 'mapichapicha' tu yaliyozoeleka kufanywa na mastaa wa Kibongo wanapokuwa wanajiandaa kufanya projekti zao mbalimbali.    

Na Mama Hamisa ambaye jina lake halisi Shufaa Lutigunga, amechochea kuni kwenye moto wa sintofahamu hiyo baada ya kuiambia Mwanaspoti leo Februari 10, 2025 kuwa hajui chochote kuhusu ndoa hiyo.

Alipoulizwa kuhusu video zilizosambaa zikitangaza ndoa hiyo, mama huyo alisema: "Jamani, jamani mimi siwezi kuzungumza kitu chochote kwa sasa, hebu tusubirini hizo tarehe zilizotangazwa zifike ndio majibu yatapatikana wala hakuna shida, halafu jamani hili ni jambo la kheri jamani na kama lipo basi tuseme Inshaallah."

HM 01

Kabla ya majibu hayo ya leo, mama wa Hamisa alizungumza na Mwanaspoti Februari 6, 2015 kuhusu habari ya ndoa hii, ambapo alisema hajapokea posa kutoka kwa Aziz Ki.

Leo katika mitandao ya kijamii imesambaa ratiba ya ndoa hiyo ya Hamisa na Aziz Ki ambayo inasomeka siku ya Februari 15, 2025, ni siku ya kutoa mahari, kisha Februari 16, 2025 ni ndoa na Februari 19 2025 ni sherehe, ambayo itarushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya Zamaradi TV.

Alipoulizwa Zamaradi Mketema, Mkurugenzi wa Zamaradi TV, ambaye ametangaza ndoa hiyo itarushwa na TV yake, amethibitisha kufanyika kwa harusi na akisema wala sio 'drama'.

"Nashindwa kuelewa kwanini baadhi ya watu wanashindwa kuamini kuwa Hamisa na Aziz Ki kama wanafunga ndoa, hii ni ndio kweli, mimi siwezi kufanya 'drama' kwenye vitu siriaz, hii ni ndoa kwa asilimia 500 nawahakikishia," amesema Zamaradi.

HM 02

"Nashindwa kuelewa kwanini baadhi ya watu wanashindwa kuamini kuwa Hamisa na Aziz Ki kama wanafunga ndoa, hii ni ndio kweli, mimi siwezi kufanya 'drama' kwenye vitu siriaz, hii ni ndoa kwa asilimia 500 nawahakikishia," amesema Zamaradi.

Mwanaspoti lilipomuuliza kama video za wawili hao wakiwa wamevaa kama maharusi sio promo za kipindi cha televisheni, Zamaradi alijibu kuwa zimerekodiwa kwa ajili ya tangazo kwamba harusi itarushwa mbashara.

"Hapana mbona picha haijakaa kama kipindi, hizo ni picha tu sababu tunarusha 'live' kwahiyo tunafanya graphics, hivyo lazima niiweke kwenye mvuto." alisema Zamaradi.

HM 03

Mwanaspoti lilipomuuliza kama video za wawili hao wakiwa wamevaa kama maharusi sio promo za kipindi cha televisheni, Zamaradi alijibu kuwa zimerekodiwa kwa ajili ya tangazo kwamba harusi itarushwa mbashara.

"Hapana mbona picha haijakaa kama kipindi, hizo ni picha tu sababu tunarusha 'live' kwahiyo tunafanya graphics, hivyo lazima niiweke kwenye mvuto." alisema Zamaradi.

Mbali na hiyo Mwanaspoti lilimuuliza Zamaradi kuhusu kadi ilivyoanza kuandikwa "Hamisa Mobetto and Aziz Ki", ilhali kikawaida huwa kwenye kadi linaanza kuandikwa jina la mwanaume anayeoa hivyo ingesomeka Aziz Ki and Hamisa Mobetto, ambapo amejibu: "hiyo ni faragha ya mtu'.

Hata hivyo, habari za ndani kutoka klabu ya Yanga Tanzania, wamedai ndoa hiyo ipo.