Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ule mtama wa Mchomvu kwa Mbasha si mchezo

Muktasari:

KATIKA tamasha la CCM, Uwanja wa Uhuru, Jumamosi iliyopita, kulitokea bonge la tukio. Mtangazaji Adam Mchomvu akamchota bonge la mtama mwanamuziki, Emmanuel Mbasha. Kijiweni kuna mjadala. Ule mtama unaitwaje? Bangi nibangue?

LUQMAN: Halafu Levy wewe bangi sana. Mtu akikwambia hivyo atarajie nini?

DK LEVY: Atarajie kicheko kikubwa sana. Maana itabidi niishie kucheka tu unadhani nitafanyaje?

LUQMAN: Kama wewe ungekuwa Adam Mchomvu, ungeitwa “Adam Mabangi” kama Adam alivyoitwa, ungeonesha busara gani tofauti na ule mtama wa Adam?

DK LEVY: Ningempuuza anayeniita hivyo pale jukwaani. Lakini, ningeongea kitu ambacho kingeeleweka kwa watu kuwa aliyeniita mimi ‘Mabange’ yeye ndo ‘Mibange’. Kwanza jukwaa lile linatazamwa na mamilioni ya watu, kuanzia pale uwanjani mpaka majumbani. Ni shoo ya bure na ikihusisha watu wa rika zote. Nisingeacha ipite bila kutoa neno la kusawazisha ili nijisafishe kwa jamii na kuifanya jamii imuone yeye anayeniita hivyo yeye ndivyo alivyo. Ila baada ya kumaliza kazi yangu pale jukwaani ningeshuka kule chini na kumalizana naye bila kamera wala kalamu za wanahabari kuona. Sasa kule chini ningemfanyaje? Inategemea na yeye, kwa sababu ningemuuliza kwanini kaniita vile kwenye jukwaa ambalo mpaka Mh. Rais anatazama, watoto, wazee, vijana, kina mama viongozi wa kidini mpaka madem zangu wa zamani na sasa. Jibu lake au mapokeo yake juu ya swali langu yangeamua nimtandike au nimsamehe. Pale jukwaani nisingemfanya lolote wala kubishana naye, hata kule chini nilikomfuata kama angeonesha kujutia ningemsamehe.

LUQMAN: Halafu kwa nini unasema ungemtandika? Kwani hana viungo ulivyonavyo? Akikutandika yeye je? Hata huyo Adam aliposema anamsaka Mbasha, vipi Mbasha angempiga? Au unamchukulia poa Mbasha?

DK LEVY: Umeuliza swali nakujibu ambacho ningemfanya unaanza kunipangia masharti ya namna ya kutoa adhabu kali ili fundisho. Sio Mbasha tu hata yeyote ambaye ningemtandika kama angekosa akili namna hii.

LUQMAN: Wewe humuwezi Mbasha akiamua kuzipiga. Sema mngepigana. By the way, Simba wamewapapua Yanga mchezaji waliyekuwa wanamlia mingo, Rally Bwalya. Simba wababe uwanjani mpaka kwenye mafioso ya usajili.

DK LEVY: Mbasha naye ile rangi yake inatoa taswira flan hivi kuwa ni rahisi kuchapika. Angalia mikono ya mtu aliyempiga mtama. Tazama miguu na mwili kwa ujumla. Kale kamwili inakuaje kamdondoshe ‘Imma’ chini alambe sakafu kama mpiga deki. Na bado anafuatwa chini kule kule aliko na anaingia unyonge? Nadhani mwanaume ukiwa mweupe sana inakupunguzia uzito wa kutisha watu na kuonekana sio mkakamavu. Unakuwa mtu unayevutia kutandikwa tandikwa mitama na mbata kama zote. Ndo maana mimi wakati nazaliwa nilikataa kupewa rangi ya mtume. Nikaacha abaki nayo dadaangu Ruth (RIP).

Any way ukiniita Levy Mibange huku mitaani wakati nipo busy kufukuzia totoz flan amazing walah nitakukata koromeo kwa vidole vyangu mwenyewe. Mbasha amekuwa mnyonge sana ingawa ule unyonge umempa ‘krediti’ kuwa alijutia kauli zake. Ila wacha nikunong’oneze hii watu wasisikie. Adam alikuwa sahihi kukasirika, ilikuwa hakuwa sahihi kumfyeka mtama. Any way ishu za Morrison na Adam zina tofauti kubwa. Kumbuka Adam ‘oldi modeli’ yule Legend alikula tunda la mti wa katikati, sijui kipi kinawafanya mshangae huyu Adam ‘nyu modeli’ kuambiwa anakula ‘bange’. Kina

LUQMAN: Achana na Mbasha, tumjadili Rally Bwalya. Hivi Yanga wanaboronga wapi? Wanachapwa kila idara. Walipigwa Nne, wakapigwa usajili wa Morrison, wametandikwa kwa Rally Bwalya. Wao wamemsajili Senzo ili akawe mshauri.

Wenzao Simba wanawekeza nguvu kwenye usajili wa wachezaji, wao wanatumia fedha na msuli mkubwa kununua mshauri.

DK LEVY: Wawa, Onyango, Bwalya, Fraga, Morrison, Konde Boy, Kagere, Deo Kanda, mchizi wake Fraga, Chama na Kahata. Wageni 11 vipi mnataka kufungua Wizara wa Mambo ya Nje au?

LUQMAN: Kanda anaondoka, anarudi kwao TP Mazembe. Shughulika na Yanga ambayo hata haifanyi usajili wa maana. Inazurura tu.

DK LEVY: Kumbe unataka nishughulike na Yanga sawa. Ila naona msemaji wenu anashughulika na Yanga kuliko Simba. Uongozi wenu unashughulika na usajili wa Yanga kuliko wenu ndo maana kila mchezaji anayetajwa na Yanga wao wanasajili. Kibaya zaidi hata wewe mfurukutwa maana sio mfuasi wala shabiki unashughulika na mambo ya Yanga. Shughulika na Simba yako.

LUQMAN: Sawa, nashughulika na Simba. Waambie Yanga wenzio kuwa akili zao zote zielekezwe kwenye usajili wa timu yao. Usilete tena habari za Harmonize na Wolper, watu wameshaachana, kila mmoja ana hamsini zake, miaka inapita, lakini hawaishi kuzungumziana. Unaona waliachana wanapendana. Ni kama Yanga, hawaachi kuizungumzia Simba. Tafsiri rahisi ni kuwa Yanga wanaipenda sana Simba ama ni vipi hapo?.

DK LEVY: Naona umenileta katika idara yangu ya ushauri wa kindoa. Hakuna mtu ambaye ni malaika, epuka kuchunguza mambo ya mtu ya nyuma...samehe, sahau na songa mbele.

Ndoa sio kitanda cha maua yanayomeremeta kila muda, ndoa zote zenye mafanikio zimepitia misukosuko mingi.

Hatuwezi kuwa sawa, kuna wa mbele na wa nyuma kidogo. Kupunguza stress, kuwa mtulivu, fanya kazi kwa bidii na kwa muda muafaka ndoto za ndoa yako zitatimia.

Ukishaoa au kuolewa ni kuingia katika uwanja wa mapambano. Kuwa tayari kupambana kuulinda ukanda wa ndoa yako.

Hakuna ndoa ambayo imetimilika. Ndoa ni kazi ngumu, jitolee mwenyewe na ufanye kazi ya kuijenga ndoa yako iwe kamilifu.

Unataka niendelee na elimu ya ndoa au unataka stori za kiki za kina Harmonize?