Tuzo za Sinema Zetu zawaibua wasanii

MSANII wa filamu Eshe Buheti ameshindwa kuvumilia kutokana na baadhi ya watu wanaolalamikia Tuzo za Sinema zilizotolewa hivi karibuni katika Ukumbi wa Mlimani City kuwa zimetolewa kwa upendeleo.
Eshe mbali na kuandika ujumbe mrefu katika akaunti yake ya instagram kuhusu kuwajibu watu wanaolalamika kuwa tunzo zimetolewa kwa upendeleo, lakini MCL Digital ilizungumza na Eshe ambapo alisema kuwa:
"Nikweli nimeandika ujumbe katika mtandao wa Inastagram na lengo ni kuwajibu wanaolalamika kuwa waliopata tunzo eti wamependelewa. Nimeamua kuandika katika mtandao wa Instagram sababu malalamiko yanatoka Instagram.
"Kwanza inabidi watu waelewe kuwa,wasanii wa filamu tuliambiwa tupeleke muvi zetu ili ziingie kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo za Sinema Zetu. Lakini tulidharau na kuendelea na mambo yetu mengine. Sasa waliopeleka za kwao na zikaingia katika michuano na kufanikiwa kushinda bado tunaleta roho mbaya na maneno maneno yasiyokuwa na maana ambayo yanavunjana nguvu.
"Tena cha ajabu wapo baadhi yetu sisi wasanii eti tunaongea ongea kama vile hatujui kilichokuwa kinaendelea na hatukufanyia kazi jamani. Watu waache kuwavunja mioyo washindi wetu. Kupitia tuzo hizo tutakuwa