Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuzo za 'HAPAWARDS' zaiva, kufanyika nchini mwezi ujao

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kilele cha tuzo hizo ni Agosti 10, mwaka huu na kwamba tayari jopo la majaji wanne waliopendekezwa ni pamoja na mmoja kutoka Hollywood na watatu wanaotokea Tanzania ambao majina yao yamefichwa


BARAZA la Sanaa Tanzania (Basata) kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania limetangaza majina ya wasanii na wadau wa sanaa wanaowania Tuzo za 'HAPAWARDS' yaani Hollywood and African Prestigious Awards.

Hayo yamesemwa leo, Julai 31,2024 ,jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Kedmon Mapana, ambapo amesema lengo la tuzo hizo zinalenga kuendelea kuwajenga wasanii na kuwapa fursa ya kujulikana kimataifa, ambapo mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro.

Amesema kilele cha tuzo hizo ni Agosti 10, mwaka huu na kwamba tayari jopo la majaji wanne waliopendekezwa ni pamoja na mmoja kutoka Hollywood na watatu wanaotokea Tanzania ambao majina yao yamefichwa.

Kwa upande wa Amberr Washington kutoka nchini Marekani, ambaye ni makamu wa rais wa tuzo hizo na pia mmoja wa waanzilishi, amesema  sababu za kuichagua Tanzania kushiriki katika tuzo ni  kusheherekea mafaniko ya sanaa nchini na kuitangaza kimataifa.

"Nimekuja hapa nchini kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya sanaa ya Tanzania pamoja na kuitangaza kimataifa," amesema Amberr.

Tuzo za HAPAWARDS zimekuwa zikitolewa kwa miaka saba mfululizo nchini Marekani ambapo kwa mwaka huu zinafanyika kwa mara ya kwanza Afrika.