Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Wakazi nakukataa, nasimama na vyombo vya habari

Muktasari:

  • Kwa kawaida msanii wa Hip Hop anapomdisi msanii mwingine yule anayedisiwa huingia studio na kutengeneza wimbo wa kujibu. Lakini mambo yalikuwa tofauti kwa Roma kwani alichukua 'screen shot' nyimbo hizo kutoka Youtube akaposti kwenye akaunti yake ya X (Twitter) pamoja na link na kuwaomba mashabiki wazisikilize. Kwa kifupi ni sawa na kusema Roma amewachukuliwa poa.

HAPO majuzi, rapa Wakazi (naamini mnamfahamu) aliachia ngoma ambayo ni Diss Track kwenda kwa Roma Mkatoliki (bila shaka mnamjua pia). Ngoma inaitwa Fall of Roman Empire. Wakati huohuo, wiki kadhaa nyuma msanii Nikki Mbishi (mnamfahamu vilevile) aliachia ngoma ya kuitwa Davinci Code Pt. 2 (Romanza) ambayo ndani pia ilikuwa na mistari kumhusu Roma.

Kwa kawaida msanii wa Hip Hop anapomdisi msanii mwingine yule anayedisiwa huingia studio na kutengeneza wimbo wa kujibu. Lakini mambo yalikuwa tofauti kwa Roma kwani alichukua 'screen shot' nyimbo hizo kutoka Youtube akaposti kwenye akaunti yake ya X (Twitter) pamoja na link na kuwaomba mashabiki wazisikilize. Kwa kifupi ni sawa na kusema Roma amewachukuliwa poa.

Kwa sababu alichofanya Roma hatujakizoea. Ni cha ajabu. Ni cha kushangaza vyombo vya habari vikaruka navyo na vikawa vinaposti kwamba Roma badala ya kujibu 'diss track' anaposti 'diss track' za Wakazi na Nikki Mbishi.

Kitendo hicho kilimkasirisha Wakazi akaandika waraka kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba vyombo vya habari vimekosa weledi. Akadai Nikki Mbishi aliachia albamu lakini vyombo vya habari havikuitangaza na mwenyewe ameachia albamu, lakini hakuna aliyeizungumzia kwenye media, lakini Roma kaposti screen shot za ngoma zao wameanza kuposti. Anadhani media zinatumika.

Kwa hapa namkataa Wakazi nasimama na vyombo vya habari. Tena namkataa kidarasani kabisa. Ukisoma uandishi wa habari kuna vitu vinaitwa misingi ya habari. Yaani ili tukio lifae kuwa habari linatakiwa kuwa na mambo matano muhimu.

Kwanza UMAARUFU: Je, hilo tukio, mtu au eneo ambalo tukio limetokea vina umaarufu mkubwa kiasi gani? Na hapa ni wazi kwamba Roma ni maarufu kuliko Wakazi. Tazama mitandao yao ya kijamii, kuanzia Insta, Twitter, Youtube ma kote. Kwahiyo media zina haki kufocus na post ya Roma.

Pili ni MUDA: Stori ni mpya kiasi gani? Au isiporipotiwa sasa hivi nini kitatokea. Post ya Roma ni tukio la mpito, lisipoongelewa muda huu litaongelewa lini? Lakini nyimbo na albamu zinaweza kufanyiwa review leo, lakini pia zinaweza kuongelea miaka 10 ijayo ikiwezekana.

Tatu UKARIBU: Je hiyo habari imetokea umbali gani na hadhira. Umbali kijographia lakini pia umbali kihisia. Tukio lililotokea Tanzania au linalomuhusu Mtanzania lina sifa ya kuwa habari kwa Tanzania kuliko tukio lilitokea Marekani. Hapa, vyote viwili, nyimbo na screenshot za Roma zinafit.

Nne LISILO KAWAIDA: Je tukio ni la kustaajabisha kiasi gani? Lina mgogoro na utata? Na je tukio ambalo tumewahi kuliona au ni jipya. Ikiwa ni jipya na la kushangaza au lisilo la kawaida hiyo inafaa kuwa habari zaidi. Kwahiyo hapa, post ya Roma inafaa zaidi ya diss track ya wakazi. Tumewahi kuona na kusikia diss track nyingi lakini hatujawahi kusikia anayedisiwa akiopush watu wakasikilize ngoma inayomdiss. Inanshangaza.

Tano MASLAHI YA WATU: Je tukio linashika hisia za jamii? Je watu wanajali kuhusu tukio hilo? Kifo cha Rais wa nchi ni habari inayobeba maslahi ya watu kuliko taarifa ya mlevi aliyepotea njia. Kwenye habari za burudani, focus yetu itakuwa ni umaarufu. Bila shaka mwenye umaarufu zaidi ndiyo anayeshika hisia za watu zaidi kwa hiyo post ya Roma inafaa kuwa habari.

Baada ya kusema hayo, pia Wakazi anatakiwa akumbuke kwamba, muziki ni biashara, huwezi kutoa nyimbo na kutegemea watu watangaze ngoma yako bila malipo. Wanaweza kufanya hivyo, lakini wasipofanya usilalamike na kuona kwamba ni haki yako vyombo vya habari kuongelea wimbo wako. Ukitoa nyimbo hakikisha una bajeti ya matangazo au ridhika na unachokipata.

Kila chombo cha habari kina aina yake ya wasikilizaji na mara nyingi huchapisha habari za kuendana na wasomaji wake. Msanii sio peke yako. Nakuhakikishia tu, kuna albamu kibao zimetoka mwezi huu lakini hutoziona zikitangazwa popote kwenye vyombo vya habari kwa sababu kwa vyombo habari, hizo sio habari.