Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Mr Blue na historia isiyowezekana

Muktasari:

  • Kwa sasa Blue ana miaka 38. Alizaliwa Aprili 1987 na kubamba kwenye muziki alibamba 2003 alipoachia wimbo wake wa kwanza unaoitwa Mr Blue. Hapo akiwa na miaka 16 tu. Tangu kitambo hicho hadi leo Blue amefanya vitu vingi vya kustahili kuwekwa kwenye historia ya muziki, lakini kikubwa ambacho watu wengi wanakichukulia poa ni ‘kuanza muziki akiwa na miaka 16 na kudumu hadi leo kwenye gemu’.

MAJUZI kati Mr Blue alikuwa anazunguka kwenye vyombo vya habari kuzungumzia jambo analotaka kulifanya mwezi huu wa nne; kuachia ngoma ishirini na mbili kwa mpigo kama sehemu ya kusheherekea miaka yake ishirini na mbili kwenye gemu. Ndiyo. Mr Blue, Bizzy Babilon, Kabaisa ametimiza miaka ishirini na mbili kwenye gemu. Si mchezo.

Kwa sasa Blue ana miaka 38. Alizaliwa Aprili 1987 na kubamba kwenye muziki alibamba 2003 alipoachia wimbo wake wa kwanza unaoitwa Mr Blue. Hapo akiwa na miaka 16 tu. Tangu kitambo hicho hadi leo Blue amefanya vitu vingi vya kustahili kuwekwa kwenye historia ya muziki, lakini kikubwa ambacho watu wengi wanakichukulia poa ni ‘kuanza muziki akiwa na miaka 16 na kudumu hadi leo kwenye gemu’.

Hicho sio kitu cha kuchukulia poa kwa sababu kipo karibu na HAIWEZAKANI kuliko unavyofikiria. Wasanii wengi wa muziki walioanza wakiwa na umri wa miaka 16 kama Blue hawakudumu kwenye gemu kwa miaka 22 na hii ni kote - ndani na nje ya nchi. Wengi waliishia kumezwa na mzigo wa ustaa katika umri mdogo. Wengi walitekwa na bata, starehe, pisi kali, pombe, madawa na gemu ikawashinda mapema tu, lakini sio Blue. Mr Blue bado anadunda.

Wasanii wengi maarufu wamevuka miaka 20 kwenye gemu, lakini walianza muziki wakiwa watu wazima. Kwa hiyo pengine utu uzima uliwabeba. Blue ameanza akiwa mtoto. Sasa chukua akili za utoto jumlisha umaarufu kisha niambie unapata jibu gani kama sio majanga. Lakini Blue ameyashinda yote hayo na anadunda hadi leo. MAAJABU.

Na hapa hatusemi kwamba Blue hajafanya starehe, hapana. Mwenyewe anakiri kwamba amezifanya sana na hicho ndicho kinafanya kudumu kwake kuwe na thamani zaidi. Kusimama kwenye gemu kwa zaidi ya miongo miwili kunahitaji kazi ya ziada. Muziki unabadilika kila kukicha. Ladha mpya zinatambulishwa. Wasanii wapya wanapokonya viti wakongwe na wakongwe wanagombana na wasanii wapya kila siku kwenye mitandao ya kijamii. Lakini, Blue bado yupo na bado anaishi na wasanii wote - wakongwe wenzake na wapya.

Yupo kwa miaka 22 kwenye gemu, lakini bado wasanii wa kizazi kipya wanamsaka kufanya naye kolabo. Hata hivyo, hatuwezi kujidanganya kwamba bado Mr Blue ana nguvu ileile aliyokuwa nayo zamani kwenye gemu, hapana. Nguvu imepungua. Lakini, pia hatuwezi kuchukulia poa ukweli kwamba bado anafanya muziki wa kiushindani na wa kibiashara ambao unamuweka mjini. Bado anafanya muziki wa kiushindani na kibiashara ambao unafanya online media zikimhoji asiwe kituko kama wakongwe wengine tunaowaona kwenye ‘TV za Youtube’, online media zikienda kumhoji zinamkuta yuko smart, hajalewa, hajawa teja, anahojiwa kwa respect na anajibu kwa respect, safi na salamu.

Mr Blue anatakiwa kuwa darasa la ustahimilivu, ubunifu na upendo kwa muziki. Rekodi aliyoifikia inatakiwa itumike kama mfano kwa madogo wote wanaotaka kuingia kwenye kiwanda cha burudani.