Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Mandojo anatukumbusha nini maana kioo cha jamii

Muktasari:

  • Muziki wa Mandojo na Domokaya ulikuwa mkubwa. Muziki wao ulikuwa na uhai. Ngoma kama Nikupe Nini, Dingi, Wanoko, Kazi Yake Mola ni nyimbo ambazo miaka kadhaa mbele lazima zitarudiwa na wasanii wa kizazi kijacho kama ambavyo ngoma nyingine classic zimekuwa zikirudiwa na wasanii wa kisasa.

KIFO cha mshkaji wetu Joseph Francis maarufu kwa jina la kisanii la Mandojo ni moja ya vifo vya wasanii vilivyonigusa sana kwa sababu sanaa ya muziki wa Mandojo na Domokaya nilikuwa naiheshimu.

Muziki wa Mandojo na Domokaya ulikuwa mkubwa. Muziki wao ulikuwa na uhai. Ngoma kama Nikupe Nini, Dingi, Wanoko, Kazi Yake Mola ni nyimbo ambazo miaka kadhaa mbele lazima zitarudiwa na wasanii wa kizazi kijacho kama ambavyo ngoma nyingine classic zimekuwa zikirudiwa na wasanii wa kisasa.

Kuheshimu kwangu kwa muziki wa Mandojo jumlisha aina ya kifo tunachoambiwa amefariki ndiyo sababu ya kuhisi kuguswa na msiba huu. Taarifa zinadai kwamba Mandojo alipigwa na mlinzi wa moja ya kanisa huko Dodoma akidhaniwa kuwa ni mwizi.

Waswahili wanasema kupamba jeneza hakumrudishii marehemu uhai, lakini ukweli ni kwamba staili tuliyoitumia kumuondoa duniani mshkaji wetu haitendei haki sanaa kubwa ya muziki aliyoifaya enzi za uhai wake.

Ngoma zote zile kali zilizojaa ujumbe na melodi tamutamu zilistahili aondoke kama hayati. Mandojo na mshikaji wake Domokaya walikuwa hawaingii tu studio kuimba, bali walikuwa wanaingia studio kuimba vitu vya maana kupitia muziki mzuri.

Nina uhakika hata enzi za uhai wake tungemuuliza Mandojo unapenda kuondoka duniani kwa staili gani, asingechagua staili ambayo tumemuondoa.

Lakini nikijaribu kutazama upande chanya, pengine Mandojo ameendelea kutumikia jukumu lake la kuwa kioo cha jamii hadi siku ya kifo chake.

Nasema hivi kwa sababu nilipokuwa nafuatilia mijadala kuhusu kifo chake kwenye mitandao ya kijamii watu wengi walikuwa wanalalamika juu ya tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi.

Watu wengi walikuwa wanahoji kwanini mtu unajichukulia uamuzi wa kumhukumu mtu. Kama unadhani kwamba mtu ni mwizi kwanini usitoe taarifa kwa Jeshi la Polisi kisha wao watakuja kumshughulikia kwa mujibu wa sheria?

Nasema Mandojo aliendelea kuwa kioo cha jamii kwa sababu kifo chake kimeikumbusha jamii umuhimu wa kutochukua sheria mkononi. Mandojo siyo mtu wa kwanza kufa kifo cha namna hiyo. Wapo watu wengi mtaani walikufa kwa kupigwa na raia wenye hasira kali kama wezi, lakini baadaye ikaja kugundulika kumbe hawakuwa wezi, kulikuwa na mkanganyiko tu ulijotokeza.

Pengine walisingiziwa au waliitiwa wezi kimakosa na kadhalika. Sababu zipo nyingi. Lakini watu wanakuja kugundua hilo kifo kikiwa kimeshatokea na hakuna cha kufanya kuweza kumrudishia uhai wake mtu ambao tayari alishapokonywa bila hatia.

Na hawa watu wote waliokufa kifo kama cha Mandojo stori zao zilipita kimyakimya kwa sababu hatuwajui. Kwa sababu siyo maarufu kama Mandojo. Kwa sababu siyo kioo cha jamii kama Mandojo.

Hivyo licha ya kwamba kifo cha Mandojo kitawauma na kuwagusa wapenzi wengi wa muziki wa Bongo fleva, lakini kwa upande mwingine pumzi yake ya mwisho imetumika kuipa funzo jamii kama ambavyo alitumia sauti yake kuipa funzo jamii kupitia muziki enzi za uhai wake.