Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KISHKAJI: Kwenye ung’eng’e Alikiba amecheza kama Pele

Kishkaji Pict

Muktasari:

  • Video hiyo ilipowekwa kwenye mitandao ya kijamii, majirani zetu wanaoamini wanafahamu kiingereza kuliko mtu yeyote Afrika Mashariki, Wakenya wakaanza kumcheka Alikiba na kumshambulia msanii mkubwa kama yeye inakuwaje hajui kuzungumza kiingereza.

ALIKIBA alikuwa anahojiwa na media moja ya kimataifa na Mtangazji wa Kikenya. Katika mahojiano hayo Alikiba aliulizwa swali kwa kiingereza. Naye alijibu kwa kiingereza kwa sekunde chache hivi, kisha akaamua kuendelea kwa kiswahili. Kwa hiyo kwa sababu ilikuwa ni media ya kimataifa ikabidi wamwekee sauti ya kutafsiri kwa juu ya kiingereza.

Video hiyo ilipowekwa kwenye mitandao ya kijamii, majirani zetu wanaoamini wanafahamu kiingereza kuliko mtu yeyote Afrika Mashariki, Wakenya wakaanza kumcheka Alikiba na kumshambulia msanii mkubwa kama yeye inakuwaje hajui kuzungumza kiingereza.

Alikiba alitoa jibu moja ambalo lilinifanya niseme kwa kweli sasa amekua. Alisema; “Napenda kuwaambia mimi ni mswahili na najivunia kuwa naongea kiswahili. Napata tabu kuongea kiingereza kwa sababu sio lugha niliyozoea kuongea kila wakati, lakini naweza kusikia na kuongea na tukaelewana.”

Hiki ndo kitu nimekuwa nasema kila siku. Kujua kuongea kiingereza ni jambo zuri sana na nyongeza kubwa na ya muhimu kama ukiwa nayo, lakini sio lazima. Ni kama vile ujue kuzungumza Kichina, Kiarabu, Kifaransa na kadhalika, sio lazima lakini ukiwa unaweza inaweza kuwa nyongeza nzuri.

Nawashangaa Watanzania wengi wanaowacheka wenzao kwa kutokujua kiingereza bila kutazama background. Mtu kama Alikiba amezaliwa na kukulia kwenye familia ambayo usikute mtu aliyesoma sana wakati yeye akiwa mtoto alikuwa ni kidato cha nne. Sasa ukizingatia Tanzania, kiingereza tunakikuta shule tena ya sekondari, niambie unategemea vipi mtu kama huyu ajue kiingereza kilichoonyoka kama Wayne Rooney? Ni uongo.

Shida ya watu hudhani kiingereza ni kipimo cha intelejensia au akili. Kwamba mtu akichapa ung’eng’e itakuwa ameelimika sana au amesoma sana au ana akili nyingi. Hapo ndo tunapojidanganya kwani kusema hivyo ni sawa na kusema chizi aliyepo milembe ya Uingereza ana akili kuliko Profesa wa Udsm kwa sababu… kila Mwingereza anazungumza kiingereza bila kujali amesoma au hajasoma, chizi au timamu, ana akili au kilaza.

Ubaya ni unakuta Alikiba amewazidi mafaniko watu wanaomcheka kuhusu kiingereza. So kiingereza hakijawasaidia.

Nilisema hapa majuzi wakati naongelea albamu ya Young Killer ambayo kuna nyimbo amechana kwa mistari ya kiingereza, tena kiingereza kibaya, ni bora achane tu kiswahili kwa sababu kuimba kwa kiingereza kibaya kunafanya wasikilizaji wadisconect na nyimbo yako. Hakuna haja ya kuprove mtu yeyote kwamba na wewe unajua kuimba kiingereza ikiwa hujui, siyo shida kutokujua kiingereza, imba kiswahili tutakuelewa na kama ukijiona sasa unataka kwenda kimataifa, basi jifunze kiingereza, kijue vizuri ili ukiimba uwe umenyooka.

Naomba tuelewane. Sisemi watu wasijifunze kiingereza. Hapana. Ukipata nafasi ya kujifunza lugha hususan lugha kubwa kama kiingereza itumie haraka, jifunze lugha itakusaidia kujielezea kwenye tamaduni tofauti tofauti. Ninachosema ni, kiingereza ni lugha na lugha tunazijua kutokana na tumekulia kwenye mazingira gani. Hivyo, hakuna haja ya kuwacheka watu kama Alikiba hususan wakionyesha na kukiri waziwazi wao wanajisikia uhuru zaidi kuzungumza kiswahili kwa sababu ndiyo lugha waliyozoea. Huo ndiyo ukubwa.