Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMK Wanaume Halisi, Wanaume Family WOTE Jukwaa moja

TMK Pict

Muktasari:

  • Makundi hayo maarufu yaliyoundwa na wakali kama Sir Juma Nature, Mheshimiwa Temba, Chegge Chigunda, KR Mullah na wengine yatatumbuiza katika katika msimu wa tatu wa tamasha la Wakongwe la Bongo Flava Honors, litakalofanyika Januari 31, 2025 kwenye ukumbi wa Warehouse, Masaki jijini hapa.

UNAKUMBUKA ule mtiti wa TMK Wanaume Family ‘Mapanga Shaa’ kabla ya kutengana na kuzaliwa kwa Wanaume Halisi? Sasa unaambiwa makundi hayo yatapanda kwenye jukwaa moja jijini Dar es Salaam kukumbushia makali yao yaliyowachizisha mashabiki na wapenzi wa muziki nchini.

Makundi hayo maarufu yaliyoundwa na wakali kama Sir Juma Nature, Mheshimiwa Temba, Chegge Chigunda, KR Mullah na wengine yatatumbuiza katika katika msimu wa tatu wa tamasha la Wakongwe la Bongo Flava Honors, litakalofanyika Januari 31, 2025 kwenye ukumbi wa Warehouse, Masaki jijini hapa.

Mwanzilishi wa tamasha hilo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alisema kundi hilo ndilo litafungua dimba kwenye msimu wa tatu wa Bongo Fleva Honors.

Katika misimu miwili iliyopita, tangu kuanza kwa tamasha hilo 2023, Sugu anasema tayari shoo 15 za wakongwe wa Bongo Fleva zimeshafanyika.

“Kati ya shoo hizo, 11 zimefanywa na mwanamuziki mmoja mmoja na nne zimefanywa na makundi na tunapokwenda kuanza msimu wa tano, kundi la TMK Wanaume ndilo linatufungulia dimba,” alisema Sugu na kuongeza:

“Hii itakuwa ni zaidi ya shoo, kwani ni dhahiri kwamba kadri miaka inavyosonga ndivyo ubora wa Bongo Fleva Honors unavyoongezeka.”

Alisema katika muziki wa Bongo Fleva, hakuna asiyefahamu namna kundi la TMK Wanaume lilivyoheshimisha tasnia ya Bongo Fleva.

“Hakuna ambaye hajui mchango wa TMK Wanaume kwenye muziki wa Bongo, hivyo tunakwenda kuwaheshimisha kwenye Bongo Fleva Honors,” alisema Sugu.

Wakizungumzia tamasha hilo, baadhi ya wasanii wa TMK Wanaume wamesema, ile ladha ya kundi hilo kwenye muziki inakwenda kuzaliwa upya.

Mheshimiwa Temba amesema tangu walipopata habari wao ndiyo wanakwenda kuiheshimisha Bongo Fleva Honors wamejipanga.

“Tumeanza mazoezi, tunawaahidi kazi mashabiki na nimuombe tu Brother (kaka) Sugu ahakikishe jukwaaa analifunga vizuri energy (nguvu) ya TMK Wanaume iko palepale.

“Wale mashabiki wetu wa wakati ule ambao sasa wengine wapo kazini tunawakaribisha waje waone kazi na kupata burudani,” amesema.

KR Mullah anasema safari hii ni bandika bandua kwenye tamasha hilo.

“Wanaume halisi na Wanaume Family kwa pamoja tunakwenda kutoa raha ya muziki pendwa,” amesema KR Mullah.

Doro na Rich One nao walisisitiza kutoa burudani ya tofauti siku hiyo ambayo mashabiki wao kwa muda mrefu waliikosa.

Inspekta Haroun ‘Babu’ ametamba kuwa ile burudani ambayo mashabiki wao waliikosa kwa muda mrefu inakwenda kujirudia.