Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yaandika Historia, yapata uwenyeji Miss World 2027

MAKONDA Pict

Muktasari:

  • Hatua hiyo imekuja baada ya kusainiwa kwa mkataba rasmi wa maandalizi ya mashindano hayo leo Aprili 20, 2026 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisaini kwa niaba ya Serikali.

Dar es Salaam. Tanzania imeandika historia mpya kwenye ramani ya dunia baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa mwenyeji wa mashindano ya 74 ya urembo duniani, Miss World 2027, tukio kubwa linalotarajiwa kuibadilisha taswira ya sekta ya burudani, utalii na utamaduni nchini.

Hatua hiyo imekuja baada ya kusainiwa kwa mkataba rasmi wa maandalizi ya mashindano hayo leo Aprili 20, 2026 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisaini kwa niaba ya Serikali.

Hafla hiyo pia ilishuhudiwa na Waziri wa wizara hiyo, Paul Makonda, ikihitimisha mchakato uliokuwa ukiendelea kwa muda wa maandalizi ya makubaliano (MoU) kati ya Tanzania na waandaaji wa mashindano hayo ya kimataifa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda alisema hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa Tanzania na ushahidi kuwa nchi imeanza kuchukua nafasi yake katika matukio makubwa ya kimataifa.

“Hii ni heshima kubwa kwa Tanzania, tumekuwa tukifanya kazi kwa muda kuhakikisha tunatimiza vigezo vyote vya waandaaji wa Miss World na leo tunajivunia kufikia hatua hii, mashindano haya yatafungua milango mikubwa ya utalii, uwekezaji na kuitangaza Tanzania kimataifa,” alisema Makonda.

Aliongeza maandalizi yatahusisha wadau mbalimbali wa sanaa, utamaduni na sekta binafsi ili kuhakikisha tukio hilo linakuwa la kiwango cha dunia.

Kwa upande wake, Msigwa alieleza kuwa ujio wa Miss World 2027 ni jukwaa muhimu la kuionesha Tanzania kwa dunia nzima.

“Kupata uenyeji wa Miss World si jambo dogo, hii ni fursa ya kipekee ya kuitangaza Tanzania kuanzia vivutio vya utalii, utamaduni wetu hadi ubunifu wa vijana wetu, Dunia itakuja kwetu, na tunapaswa kujiandaa kuitumia vyema nafasi hii,” alisema Msigwa.

MIS 01

Historia kwa Afrika

kwa mafanikio hayo, Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi chache Afrika kuandaa mashindano hayo makubwa ya urembo, ikiwa ni nchi ya pili baada ya Afrika Kusini.

Hatua hiyo inaendelea kuonyesha dhamira ya Serikali kuimarisha sekta ya burudani na kuitumia kama nyenzo ya kukuza uchumi, sambamba na jitihada zinazoendelea za kuiweka Tanzania kwenye ramani ya matukio makubwa duniani.

MIS 02

Msukumo mpya kwa utalii na burudani

Kwa mujibu wa wadau wa sekta hiyo, mashindano ya Miss World yana mvuto mkubwa kimataifa na huvutia washiriki na watazamaji kutoka mataifa mbalimbali, hali inayotarajiwa kuongeza mapato ya utalii na kukuza ajira.

Tayari Tanzania imeanza kuonesha mwelekeo huo baada ya kufanikisha mashindano ya kitaifa ya Miss World Tanzania 2026, yaliyovutia ushindani mkali na kuibua vipaji vipya katika urembo na utamaduni.

MIS 04

Safari ya kuelekea 2027 yaanza

Baada ya hatua hiyo ya kihistoria, sasa macho yote yanaelekezwa kwenye maandalizi ya kina ya kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa mashindano hayo.

Kwa sasa, ni wazi Tanzania haiko tena nyuma, bali imeanza kusimama mbele ya jukwaa la dunia.