Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabia za mashabiki zamkera Wema Sepetu

Muktasari:

  • Wema ameitoa ameitoa kauli hiyo, baada ya hivi karibuni mashabiki kuwashindanisha wafuasi (followers) alionao na wale wa Mabeto katika mtandao wa kijamii na kuanzishwa ligi ndogo iliyomfanya Mobetto kwa sasa kumpita Miss Tanzania huyo kwa idadi ya wafuasi waliopo akaunti zao za instagram na kuwa na milioni 11.6

MISS Tanzania 2006, Wema Sepetu amesema huwa hapendezwi na kitendo cha mashabiki kumshindanisha na mwanamitindo Hamisa Mobetto, kwani jambo hili ni kama wanamtengenezea chuki na mrembo huyo.

Wema ameitoa ameitoa kauli hiyo, baada ya hivi karibuni mashabiki kuwashindanisha wafuasi (followers) alionao na wale wa Mabeto katika mtandao wa kijamii na kuanzishwa ligi ndogo iliyomfanya Mobetto kwa sasa kumpita Miss Tanzania huyo kwa idadi ya wafuasi waliopo akaunti zao za instagram na kuwa na milioni 11.6

"Naomba nifikishie ujumbe sitaki,i kushindanishwa na mtu kwa kitu chochote, sijawahi kushindana na mtu yeyote tangu nianze kupata umaarufu mwaka 2006, na sipendezwi kabisa kitendo cha kushindanishwa na Hamisa Mobetto kwani yule ni mdogo wangu halafu mtaleta chuki ambazo hazina maana," alisema mkali huyo wa Bongo Movie.

Kwa muda mrefu, Wema  amekuwa mtumiaji wa Instagram wa hapa Tanzania mwenye wafuasi wengi katika mtandao huo akiwa na wafuasi milioni 11.5, huku Hamisa Mobetto akiwa wa pili kwa kuwa na Milioni 10 kabla ya hivi karibuni kumpita akifikisha Milioni 11.6.