Swahili Comedy waja na mpango mpya

KIKUNDI cha  wachekeshaji kimekuja na mkakati mpya wa Comedy Club ambao utaunganisha wachekeshaji wote Tanzania.

Hii itakwenda kuwajenga katika Sanaa ya Uchekeshaji na kuwa bora zaidi kwani watakuwa na mazoezi ya kutosha ambayo watayafanya kila mara hapa maeneo ya Swahili.


Mfumo huu utawawezesha Wachekeshaji wote kujulikana kwani watakuwa na awamu ya kupanda jukwaani.


Mchekeshaji Maxwel Machange, alizungumza na Mwanaspoti alisema waliamua kuunda jambo hili ili kukuza vipaji na lengo ni kuhakikisha wanaifanya kama kazi kwa vijana wengi.


Aidha alisema watazingatia maadili ili kutokuvunja sheria na kufanya iwe kazi ya heshima kama ajira zingine ili kujikwamua kiuchumi.


“Vijana wengi ambao wanavipaji vya kuigiza watapata fursa ya kuingiza kipato na kufahamika zaidi nje na ndani ya Nchi,”

“Sasa imekuwa kazi ambayo inawainua  wengi hivyo wote wenye vipaji wakaribie na kuonyesha kile walichonachao na tutawapa nafasi na kusaidiana kama vijana.”alisema Mchekeshaji Machange

Aliendelea kusema jambo hili litakuwa endelevu na ni kazi ya kuheshimiwa kama zingine hivyo itaanza rasmi tarehe 27/5.