Steven Nyerere agoma kung'oka bila barua

Muktasari:
- Wakati sakata la kumtaka msanii Steven Mengele maarufu Steve Nyerere, kujiuzulu nafasi ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), mwenyewe amesema hatojiuzulu hadi aandikiwe barua na waliomteua.
Dar es Salaam. Wakati sakata la kumtaka msanii Steven Mengele maarufu Steve Nyerere, kujiuzulu nafasi ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), mwenyewe amesema hatojiuzulu hadi aandikiwe barua na waliomteua.
Akizungumza leo Jumanne Machi 22, 2022 na waandishi wa habari Steve amesema hatajiuzulu hadi pale waliomteua watakapompa barua kama walivyofanya wakati akitaka atumikie nafasi hiyo.
"Mimi siwezi kung'oka kihuni huni, kwa kuwa nafasi hii nimeteuliwa tena kwa barua, halafu anakuja mtu anasema anatoa saa 48 nijiuzulu. Yeye nani sitafanya hivyo labda uongozi unipe barua ya kutengua nafasi yangu," amesema Steve.
Katika hatua nyingine msanii huyo ambaye alikuwa akisema anazungumza kama msemaji wa Shirikisho hilo amewapa saa 48 wasanii waliotoa maoni yao jana kwa dhihaka ikiwemo kuuita uongozi 'Zumaridi Gang' kuomba msamaha.
Sakata la kutaka Steve Nyerere aondolewe katika nafasi hiyo lilianza wiki iliyopita mara tu baaa ya kutangazwa na uongozi wa Shirikisho hilo na jana katika kikao cha kupokea maoni kwa wanachama kuhusu maamuzi hayo.