Shilole kufanya kolabo na Koffi Ufaransa

Friday November 27 2020
shilole pic
By Nasra Abdallah

KITENDO cha msanii Koffi Olomide kwenda kula kwenye mgahawa wa msanii Shilole, hakikuishia kwenye kula bali na kuzungumzia kazi.

Hayo ameyaeleza Shilole ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed, alipokuwa akiitambulisha kwa waandishi wa habari lebo ya Shishi Gang  na msanii wa kwanza kumsaini.

Pamoja na mambo mengine, Shilole alielezea matunda ya kutembelewa na msanii huyo kwenye mgahawa wake siku mbili zilizopita.

"Nashukuru ujio wa Koffi hakuniacha hivi hivi, kwani tumezungumza mengi ikiwemo kwenda kutengeneza naye kolabo nchini Ufaransa, amenipa mualiko maalum na amesema tutarekodia studio kwake na nitafikia kwenye hoteli yake ya nyota tano anayoimiliki nchini humo," amesema Shishi.

Msanii huyo ambaye awali katika ukurasa wake aliandika kumshukuru Diamond kumpelekea msanii huyo na kueleza sio mara ya kwanza kumpelekea wasanii.

Aliwataja wasanii wengine ambao amewahi kumpelekea kuwa ni pamoja na Wizkid na Tiwa Savage.
 

Advertisement
Advertisement