Shilole afunga ndoa ya tatu

Thursday April 22 2021
shishi pic
By Nasra Abdallah

Hatimaye msanii Zuwena Mohamed maarufu Shilole ameolewa na mpiga picha wake Rommy 3D.

Jambo hilo limebainishwa na Shilole leo Alhamisi Aprili 22, 2021 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.

Hii itakuwa ndoa ya tatu kwa msanii huyo, ambaye miezi saba iliyopita aliachana na aliyekuwa mume wake Ashraf Uchebe kwa kile alichoeleza kuchoshwa na vipigo vya muda mrefu  kutoka kwa mwanaume huyo.

Baada ya kuvunjika kwa ndoa hiyo, alianzisha mahusinao mapya na mpiga picha wake Rommy 3d.

Katika ukurasa wake leo amweka picha za harusi na kuandika "Alhamdulillah tumemaliza salama, rasmi mke na mume.

"Nimechukuliwa kwa furaha na kwa mapenzi mazito, kwa sasa unaweza kuniita mke wa Rajab Issa (Rommy).Yarab iwe Salama,"

Advertisement

Baadhi ya wasanii walimpa hongera kwa hatua hiyo akiwemo msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu kwa kuandika " Kwa hiyo umenivja ubibi harusi, hongera mama,"

Wengine ni wasanii wa muziki wa Bongofleva Nandy ambaye ameandika "Weuweee umenogaaa,".

Wakati Billnass ameandika "Hongera sana Shishi, ikawe heri,".

Wakati Profesa Jay ameandika "Waoo hongera sana mdogo wangu Mwenyezi Mungu awe msimamizi wenu mkuu wa ndoa yenu, idumu siku zote za maisha yenu,"

Advertisement