Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka 10 kabla ya Shakira na Gerard Pique!

SHAKIRA Pict

Muktasari:

  • Ikumbukwe Shakira na Pique walikutana kwa mara ya kwanza huko Madrid, Hispania wakati wakitayarisha video ya wimbo maalamu wa Kombe la Dunia 2010, Waka Waka (This Time for Africa).

MAISHA binafsi ya mwanamuziki kutokea Colombia, Shakira, 48, yamejadiliwa sana kwa miaka mingi na kati ya yaliyomuweka katika vichwa vya habari ni uhusiano wake na Gerard Pique, 38, mwanasoka wa zamani.

Hata hivyo, Shakira aliyevuma na kibao chake cha Hips Don’t Lie (2005), kabla ya kukutana na mchezaji huyo wa Hispania na FC Barcelona alishakuwa katika uhusiano mwingine uliodumu kwa miaka 10!

Ikumbukwe Shakira na Pique walikutana kwa mara ya kwanza huko Madrid, Hispania wakati wakitayarisha video ya wimbo maalamu wa Kombe la Dunia 2010, Waka Waka (This Time for Africa).

SHAKI 01

Wakati huo Pique alikuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichoshinda Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, michuno ambayo Shakira alitumbuiza katika sherehe za ufunguzi.

Baada ya miaka zaidi ya 10 uhusiano ulioangaziwa sana na vyombo vya habari na mitandao, hatimaye Juni 2022, wawili hao wakatangaza kuachana wakiwa tayari wamejaliwa watoto wawili, Milan (2013) na Sasha (2015).

Uhusiano wa Shakira na Pique ulikuja baada ya mwanamuziki huyo kuachana na mtoto wa Rais wa zamani wa Argentina, Fernando de la Rua ambaye aliiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1999 hadi 2001.

SHAKI 02

Huyu si mwingine bali ni Antonio ambaye uhusiano wake na Shakira ulianza mwaka 2000 hadi Januari 2011 walipoachana rasmi baada ya migogoro mingi ya kikazi na kibiashara.

Wawili hao walitengana hapo Agosti 2010 katika kile walichoeleza ni uamuzi wa pande zote mbili ila Antonio akaendelea kusimamia biashara na masilahi ya kazi za sanaa za Shakira kama ambavyo alikuwa akifanya.

Shakira, Malkia wa Muziki wa Kilatini, mnamo Januari 10, 2011, kupitia tovuti wake ndipo alitangaza kuachana na Antonio na kueleza kile walichokubaliana kwa pamoja baada ya miaka 10 ya uhusiano wao. 

SHAKI 03

“Tangu Agosti 2010 tumekubaliana kwa pamoja kuchukua muda kuwa mbali na uhusiano wetu wa kimapenzi,” Shakira alieleza na kuendelea: “Katika wakati wote tumeendelea kufanya kazi pamoja, tumebakia kuwa karibu na kuweka faragha masuala yote”. 

“Sote tunakitazama kipindi hiki cha kutengana kama cha muda tu, na muda wa kila mmoja kukua huku tukiendelea kama washirika upande wa biashara,” sehemu ya taarifa ya Shakira ilieleza.

Lakini kwa Antonio mambo hayakuisha kwa urahisi hivyo kama bibie alivyotaka - alimburuza Shakira mahakamani akidai haki yake akitaka kulipwa kiasi kikubwa cha fedha!

SHAKI 04

Mnamo Septemba 2012, Antonio alimshtaki Shakira akidai fidia ya Dola100 milioni, wastani wa Sh245.7 bilioni kwa sasa, kwa kile alichodai alichangia sehemu kubwa ya mafaniko ya mwimbaji huyo.

Kati ya dili ambazo Antonio alikuwa anadai kuzileta kwa Shakira ni ile na kampuni ya matamasha, Live Nation yenye thamani ya Dola300 milioni, dili ambalo mkataba wake ulikuwa wa miaka 10.

Shakira alipinga hilo akisema alifanya kazi na Antonio kama mshauri wake wa kibiashara na alilipwa kwa kazi hiyo. Na kufikia Agosti 2013, mahakama ya juu huko Los Angeles, Marekani alitupilia mbali kesi hiyo.

SHAKI 05

Ni wazi Antonio alikuwa na mchango mkubwa katika muziki wa Shakira, tangu walivyoanza kuwa pamoja mwaka 2000, mwanamuziki huyo alivumbua masoko mapya kwa albamu kali zilizofanya vizuri.

Walikuwapo pamoja wakati msanii huyo anatoa albamu yake ya kwanza ya Kiingereza na ya tano kwa ujumla, Laundry Service (2001) iliyouza nakala zaidi milioni 13 duniani kote.

SHAKI 08

Albamu zake nyingine za Kiingereza kama Oral Fixation, Vol. 2 (2005), She Wolf (2009) na Shakira (2014) zote zilifikia mauzo ya Gold. Kwa Marekani mauzo ya Gold yana maana kazi husika imeuzwa au kusikilizwa kwa kiwango kinacholingana na nakala 500,000.

SHAKI 06

Na hata albamu zake za Kihispania, Fijacion Oral, Vol. 1 (2005), Sale el Sol (2010) na El Dorado (2017), zilifanya vizuri katika chati Kilatini za Billboard, na kufikia mauzo ya Platnum (nakala milioni 1).

Hivyo, Antonio ambaye aliwahi kuwa mshauri wa Rais Fernando de la Rua, ni kama alikuja kuipa nguvu nyota ya Shakira kimuziki maana tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 ndipo mwimbaji huyo alivuma sana.

Kwa sasa Shakira akikadiriwa kuuza rekodi kati ya milioni 80 hadi 95, anatajwa kama msanii wa kike wa Kilatini aliyeuza zaidi kwa wakati wote, huku akiwa ameshinda tuzo nne za Grammy, na 15 za Latin Grammy.

SHAKI 07

Mwaka 2018, Spotify ilimjumuisha katika orodha ya wasanii 10 bora wa kike waliosikilizwa zaidi kwa muongo huo kwenye mtandao huo na kumfanya kuwa msanii wa Kilatini aliyesikilizwa zaidi.

Na miaka miwili baadaye, Shakira akaweka rekodi kama msanii wa kwanza wa kike kuwa na nyimbo nne kutoka miongo tofauti kusikilizwa (streams) zaidi ya mara milioni 100 Spotify. Kwa ujumla anashikilia nafasi ya tatu baada ya Michael Jackson na Eminem.