Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rayvanny afunguka kwanini hakumuiga Harmonize kujitoa Wasafi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny ameandika historia ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuanzisha lebo ya muziki ikiwa bado anafanya kazi chini ya lebo nyingine.

Rayvanny ambaye anatamba na albamu yake ya Sound from Africa alizindua lebo yake  inayoitwa Next Level Music Machi 9 akiwa bado ni msanii anayefanya kazi chini ya lebo ya Wasafi, hiyo ikiwa ni tofauti na msanii Harmonize ambaye alijitoa Wasafi mwaka 2019 na kwenda kuanzisha lebo yake ya Konde Gang.

Akizungumza na Mwananchi Rayvanny amefichua kwanini hakufuata njia za Harmonize ambapo amesema ni kwa sababu anaamini muziki ni biashara ambayo hufanikiwa pale inapofanywa na timu.

"Hata nikitoka Wasafi leo nitaenda kutengeneza timu nyingine ya kunisaidia kazi, sasa kwanini nifanye hivyo ikiwa timu niliyonayo bado ina nguvu ya kunipeleka mbali. Hata waliotoka Wasafi wamekwenda kutafuta watu wengine wa kufanya nao." alisema Rayvanny.

Aliongeza kuwa ameanzisha lebo yake kwa ajili ya kusaidia vijana wengine mtaani wenye vipaji kama ambavyo yeye alisaidiwa na Babu Tale, Madee na Mkubwa Fela.

"Nilipokuja Dar sikuwa na ndugu, nilikuwa na nguo moja tu. Lakini kwa sababu nina kipaji, watu ambao hata sio ndugu zangu ndio walionishika mkono na kunifikisha hapa. Nataka kufanya hivyo pia, nataka kuona Rayvanny wengine wanatoka mikononi mwangu." Alisema.

Hafla ya uzinduzi wa lebo hiyo ilifanyika kwa ajili ya kuonyesha ofisi pamoja na studio zake zilizopo Mbezi Beach, Dar es Salaam lakini siku chache zijazo atatambulisha wasanii wa lebo hiyo.