Mbosso kuachia albamu, Rayvanny akifungua lebo yake

Machi kumekucha WCB. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya wasanii wawili kutoka lebo hiyo kutarajia kufanya mambo makubwa kwenye muziki wao.
Wasanii hao ni Mbosso na Rayvanny ambapo kwa siku ya leo Jumanne, Machi 9,2021 watakuwa na matukio tofauti yatakayewasogeza kutoka hatua moja kwenda nyingine katika kazi yao ya muziki.
Mbosso ambaye jina lake halisi ni Yusufu Mbwana, tayari ametangaza kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki na pia alipojiunga na lebo ya WCB.
Mbosso kabla ya kwenda WCB alikuwa moja ya wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto lililokuwa na wasanii kama Aslay, Beka Fleva na Enock Bella, ambalo lilivunjika mwaka 2017 na kila mtu kuanza kufanya kazi kivyake.
Tangu ameingia katika lebo hiyo mwaka 2018, msanii huyo amekuwa moto wa kuotea mbali hii ndio mara ya kwanza anaachia albamu licha ya kuwa na nyimbo nyingi.
Albamu hiyo ameipa jina la ‘Definition of Love’, ambayo ina nyimbo 12 na kati ya hizo hakuna hata moja ambayo ni kati ya nyimbo alizowahi kuzitoa huko nyuma.

Kwa upande wa Rayvanny tayari ameteyangaza leo usiku kuwa na tukio la kuzindua lebo yake aliyoipa jina la ‘Next level Music’.
Pia tayari msanii huyo hivi karibuni aliachaia albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Sound from Africa’ ambayo inafanya vizuri katika mitndao mbalimbali ya kuuzia kazi za muziki.
Ujio wa lebo hiyo kwa Rayvany, utafanya kuwa msanii wa pili kuwa na lebo, huku akitanguliwa na Harmonize ambaye alijiengua mapema mwaka juzi na kuanzisha lebo yake ya Konde Gang ambayo mpaka sasa ina wasanii watano.