Rais Samia ataja sababu kushiriki ‘The Dream Concert’, azindua kitabu cha Sugu

Tuesday May 31 2022
sugu pic3

Rais Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabu cha Msanii Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu za kukubali kushiriki kwenye tamasha la msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ‘The Dream Concert’ huku akizindua kitabu cha muziki na maisha cha mwanamuziki huyo.

Tamasha hilo limefanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam likiwa ni maalumu kwa mbunge huyo wa zamani wa Mbeya Mjini kuadhimisha miaka 30 kwenye sekta ya muziki.

Akieleza sababu ya kukubali kushiriki tamasha hilo, mkuu huyo wa nchi ameweka wazi sababu mbili akisema "Kwanza kwa Joseph mimi ni mama hivyo niliona fahari kushuhudia mafanikio ya mwana”

sugu pic2

Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa muziki wa Hiphop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mara baada ya kuwasili Serena kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la maadhimisho ya miaka 30 ya msanii huyo. Picha na Ikulu

Akitaja sababu ya pili, Rais Samia amesema "Lakini pia nilivutiwa na wazo la kuandika kitabu, nikasema naenda kumsapoti, japo tarehe aliyoipanga mwanzo nilikuwa bize, akasema atasogeza mbele na leo niko hapa na nitazindua kitabu chake," amebainisha

Akitaja majina ya utani ya mwanamuziki huyo likiwamo la Taita na Sugu ambalo alisema hawezi kumuita kwa kuwa sasa mwanamuziki huyo huku akikumbusha moja ya tukio la Sugu lililotokea bungeni wakati mkali huyo wa HipHop akiwa anawawakilisha wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini.

Advertisement

"Mimi nitamuita Joseph, nakumbuka siku alipomuudhi Spika akasema mtoeni nje, alishikwa mguu na mkono," amesema Rais Samia.

Amesema safari ya Sugu kwenye tasnia muziki haikuwa rahisi, aliingia wakati bado muziki ukiwa haukubariki.

Katika tamasha hilo, Rais Samia aliweka wazi kuwa kuna kipendi hata yeye alikuwa mtazamo kuwa mziki wa HipHop ni uhuni huku akieleza kuwa mtazamo huo umebadilika.

"Hata mimi nilipokuwa nikiwaona wanafoka foka niliona uhuni wakati ule, lakini kumbe sio kweli, muziki umeleta heshima," amesema.

sugu pic1

Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Serena pamoja na msanii wa muziki wa Hiphop nchini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu

Amesema muziki wa Hip Hop hauna maneno ambayo huwezi kusikiliza ukiwa na watoto.

"Hapa wasanii wameimba sijasikia maneno ya kukera, nimeona wabunge na wakuu wa wilaya wakiimba, nikajiuliza wanafanya kazi saa ngapi, lakini wanajua wanavyojigawa, simvunji moyo, nimebariki aendelee tu," amesema.

Rais Samia alizindua zinduzi wa kitabu cha msanii  huyo chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika tamasha hilo.

Katika hafla hiyo, Rais Samia alimuita Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jukwaani na viongozi wengine wakati wa kuzindua kitabu cha Maisha na Muziki cha Sugu.

Wengine waliopanda jukwaani na Rais Samia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mpainduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Mohammed Mchengerwa na Sugu na mkewe.

Advertisement