P the Mc na Ep mjini

MSANII wa mziki wa Hip Hop nchini, Cleofas Yesaya 'P the Mc' ameachia Ep yake ya kwanza yenye jina la matukio ya simu ikiwa na nyimbo nane.

Katika Ep hiyo msanii huyu ametumia zaidi kuelezea namna ambavyo simu inavyokuwa na matukio hasa kwenye makundi ya mtandao wa WhatsApp pamoja na namna ambavyo wapenzi wanavyokutana.

P the Mc moja ya nyimbo ambazo ameimba ni namna ambavyo amekutana na msichana kwenye mtandao wa Instagram na hilo ni kutokana na kuwa na simu ya mkononi.

"Kwenye mtandao picha kali, kukutana nae ni kituko bwana, amejipaka mapoda mengi na nilipomuuliza akadai zile picha za sista," ni sehemu ya mashairi ya kwenye wimbo huo.

Akizungumzia Ep yake, P The Mc amesema;"Haikuwa kitu cha haraka sana, nilitumia muda mwingi sana kuandaa kitu kilicho bora na ndio maana nimeachia wakati huu."