P Diddy awatoroka polisi,watoto wake wakamatwa

Muktasari:

  • Uchunguzi huo uliongozwa na mawakala wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI). Tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Diddy ni zile zilizoanza kuvuma tangu mwaka jana.

Makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami jana Jumatatu , Machi 25, yamefanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

Uchunguzi huo uliongozwa na mawakala wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI). Tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Diddy ni zile zilizoanza kuvuma tangu mwaka jana.

Hata hivyo, katika upekuzi huo, watoto wawili wa kiume wa Diddy, Justin na King Combs, walitiwa mikononi mwa askari.  Jumba la Diddy lililofanyiwa upekuzi ni lile ambalo alizindulia albamu yake ya mwisho mwaka jana (The Love Albam Off the Grid).

Utakumbuka kuwa mpenzi wa zamani wa Diddy, Casandra Ventura, maarufu kwa jina Cassie, aliwahi kumshutumu Diddy kwa kumbaka na kumshambulia mara kwa mara na kusema alimlazimisha kufanya mapenzi na wanaume mbele yake.

Pia Joi Dickerson-Neal alimshutumu Diddy kwa kumpa dawa za kulevya na kumbaka mwaka wa 1991. Si hivyo tu zipo tuhuma nyingine pia za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili nyota huyo

Kwa mujibu wa jarida la 'People' ndege binafsi ya ya P Didy iliyoonekana katika visiwa vya Caribbean haikuwa ya Rapa huyo hii ni baada ya msanii huyo kuzuiwa kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Opa-Locka uliopo Miami Marekani.