Video 10 za Bongofleva zilizoshutiwa nchi mbili tofauti
Muktasari:
- Baadhi ya nyimbo hulazimisha hilo kufanyika, na nyingine ni matakwa na utashi binafsi wa wasanii wenyewe. Kwa kulitambua hilo tunakuleta video 10 za Bongofleva ambazo zimeshutiwa katika nchi mbili tofauti.
Kwa miaka mingi wanamuziki wa Bongofleva wamekuwa na utamaduni wa kusafiri nchi mbalimbali kwa ajili ya kutengeneza video za nyimbo zao, jambo ambalo huongeza thamani ya kazi hizo.
Baadhi ya nyimbo hulazimisha hilo kufanyika, na nyingine ni matakwa na utashi binafsi wa wasanii wenyewe. Kwa kulitambua hilo tunakuleta video 10 za Bongofleva ambazo zimeshutiwa katika nchi mbili tofauti.
1. Rayvanny - Teamo (202o), Sehemu aliyoimba Rayvanny katika wimbo huu imeshutiwa Tanga, Tanzania, na kipande cha mwimbaji wa Msumbiji, Messias Maricoa aliyeshirikishwa kimefanyika Lisbon, Ureno.
2. Shilole - Malele (2015), Mwimbaji huyu alienda Ubelgiji kufanya show ndipo akaaanza kushuti video ya wimbo huo kabla ya kwenda kumalizika vipande vinginne huko Amsterdam nchini Uholanzi.
3. Diamond Platnumz - Utanipenda (2015), Video hii ambayo aliyekuwa mpenzi wa mwimbaji huyo, Zari The Bosslady alitokea, imeshutiwa Dar es Salaam, Tanzania, na Johannesburg, Afrika Kusini.
4. Roma - Diaspora (2020), Sehemu aliyopo Roma katika video hii ni Massachusetts, Boston nchini Marekani, na Lady Jaydee ambaye ameshirikishwa yeye yupo Bagamoyo, Tanzania huku kile eneo likiwa na director wake.
5. Mr. Blue - B.L.U.E (2019), Nandy akiwa ameshirikishwa ndani yake, video ya ngoma hii imefanyika Tanzania pamoja na Afrika Kusini chini Director Msafiri a.k.a Levels Baba kutokea Kwetu Studios.
6. Lady Jaydee - Popo Remix 3 (2025), Akiwashirikisha Rapcha na Frida Amani, watatu hao walishuti Tanzania, ila Wakazi ambaye naye amesikika katika wimbo huo yeye kipande chake ameshuti akiwa Marekani.
7. Nandy - Dah Remix (2024), Wimbo huu ambao Nandy amewashirikisha G nako, Joh Makini, Rosa Ree, Moni Centrozone na Stamina, hawa walishuti Dar es Salaam ila Khaligraph Jones yeye sehemu yake ilishutiwa kwao Nairobi, Kenya.
8. Rostam - Sifa (2021), Kundi hili la Hip Hop linaloundwa na Roma na Stamina, lilimshirikisha Ben Pol katika wimbo huu. Roma yeye alishuti kipande chake akiwa Marekani, huku Stamina na Ben Pol wakifanya hivyo wakiwa Tanzania.
9. Mbosso - Shilingi (2019), Wimbo huu ambao Mbosso alimshirikisha Reekado Banks kutokea Nigeria, video yake imeshutiwa Dar es Salaam, Tanzania, na Nairobi, Kenya.
10. Jux - Umeniweza (2020), Video hii ambayo mpenzi wa zamani Jux, Nayika alitokea, imeshutiwa Bali nchini Indonesia, pamoja na Serengeti, Tanzania huku kila nchi ikiwa na director wake aliyesimamia eneo husika