Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz, kuna Wema Sepetu

MISS Tanzania 2006, Wema Sepetu kwa miaka kadhaa amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa mambo mengi, kuanzia urembo na mitindo, filamu, mahusiano yake na mengineo yenye kuacha maswali kuhusu mtindo wake wa maisha.

Hata hivyo, hiyo haiondoi ukweli kwamba Wema ana nguvu ya ushawishi na ndio sababu kila analofanya au kujiri katika maisha yake, basi linateka mazungumzo.

Staa wa Bongofleva kutokea WCB Wasafi, Diamond Platnumz na mashabiki wake wanaijua vizuri nguvu ya Wema katika kuikuza na kuitangaza chapa ya msanii huyo kipindi akipigania mafanikio yake ya awali katika tasnia.

Utakumbuka baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania, Wema alishiriki mashindano ya urembo ya dunia (Miss World) kule Warsal, Poland ila hakufanya vizuri. Miss. Baada ya kukabidhi taji, Wema alieleka nchini Malaysia aliposomea Biashara ya Kimataifa (International Business) katika Chuo Kikuu cha Limkokwing, aliporejea akajitosa katika uigizaji.

Filamu yake ya kwanza  ni; A Point of No Return (2007) akiwa na Marehemu Steven Kanumba, kisha zikafuata; Family Tears (2008), Red Valentine (2009) na White Maria (2010), kazi hizi zilimfanya kuwa maarufu zaidi.

Huyu ndiye mwanamke wa kwanza Tanzania kufikisha wafuasi (followers) 1 milioni Instagram (2015), huku Diamond akiwa wa kwanza upande wa wanaume, kwa mtiririko kamili alianza Diamond, Wema, Millard Ayo kisha Jokate Mwegelo.

Na baada ya miaka saba (2022) Wema akawa wa kwanza tena kufikisha wafuasi milioni 10 Instagram akiwa ni mwanamke wa pili Afrika Mashariki baada ya Zari The Bosslady (Uganda), waliomfuatia Wema ni Lupita Nyong’o (Kenya), Hamisa Mobetto na Shilole (Tanzania).

Kitendo cha Wema kuwa na uhusiano na Diamond, kilipelekea jina la mwanamuziki huyo kukua kwa kasi katika Bongofleva, Wema alimrithisha Diamond umaarufu kipindi ambacho ndipo tu ameachia nyimbo zake, Kamwambie na Mbagala (2009).

Ikumbukwe Wema ambaye kwa sasa yupo na staa mwingine wa Bongofleva, Whozu, kabla ya kuwa na Diamond, tayari alikuwa na uhusiano na wanamuziki wengine ambao ni Mr. Blue, TID na Chaz Baba.

Diamond na Wema walipendana sana ingawa uhusiano wao iligubikwa na drama nyingi lakini hilo haliondoi ukweli kwamba Wema alimjenga Diamond kimuziki, alimfundisha Lugha ya Kiingereza na kumpa hasira ya mafanikio. Wema alitokea kwenye video ya wimbo wa Diamond, Moyo Wangu (2011), huku Diamond akimtungia wimbo, Lala Salama (2012), na kwa ujumla Diamond amemtaja Wema katika nyimbo zake kama; Nimpende Nani (2012), Kesho (2012) na Fire (2017).

Utakumbuka Wema ndiye ameingiza sauti za chini (back vocal) katika nyimbo za Diamond, Chanda Chema na Lala Salama, pia amefanya hivyo katika wimbo wa Marehemu Haitham Kim, Play Boy.

Mafanikio ya Diamond kimuziki kwa kipindi cha miaka 13 iliyopita yameitangaza na kuikuza Bongofleva, lakini huwezi kuacha kumtaja Wema Sepetu kwa namna moja ya nyingine.

Wema ndiye Miss anayeuza zaidi katika Bongofleva, wasanii wanashindana kutaja jina lake katika nyimbo zao, waliofanya hivyo ni Tundaman - Sio Demu (2012), Young Killer -  Mrs Superstar (2013), Nikki Mbishi - Kill Your Self (2013) na Gosby - Wema Sepetu (2015).

Wengine ni Rayvanny - Natafuta Kiki (2016), Fid Q -  Sumu (2016), Alikiba - Aje (2017), Aslay - Natamba (2017), Rostam - Hivi Ama Vile (2017), Joh Makini - Mchele (2019), Harmonize - Mtaje (2021), Marioo - Tomorrow (2023) n.k.

Ikumbukwe chini ya kampuni yake, Endless Fame, Wema alifungua lebo ya muziki, Endless Fame Label (2016) na kuwasaini wasanii wawili, Mirror na Ally Luna, kupitia Endless Fame Label ndipo akamuibua Lulu Diva aliyetokea katika video ya Mirror, Naogopa (2016). 

Kwa ufupi Wema alifungua milango kwa wasanii wa kike Bongo kuwa na rekodi lebo zao, waliofuta nyayo zake ni Vanessa Mdee (Mdee Music), Shaa (SK Music), Nandy (The African Princess Label), Shilole (Shishi Gang) na Hamisa Mobetto (Mobetto Music).