Nyimbo za Ali Kiba zilivyombeba Whozu

Nyimbo za Ali Kiba zilivyombeba Whozu

Msanii wa Bongofleva maarufu kama Whozu, amesema kabla hajatoboa kimuziki alizitumia  nyimbo nyingi za staa Ali Kiba kujifunza namna ya kuimba.

Whozu amesema japokuwa wapo wasanii wengi anaowakubali, lakini nyimbo za Ali Kiba aliziimba kila siku na alitamani kufika levo zake za kimuziki.
"Nyimbo ya Ali Kiba ya Cinderella nimeiimba sana, kuna wakati nilikuwa naenda kufanya mazoezi baharini ama nikiwa nyumbani ilikuwa lazima nitaimba tu," amesema Whozu na kuongeza;

"Niliwahi kumwambia Ali Kiba nilikuwa naimba sana nyimbo zake, alifurahi sana na aliniambia tutafanya kazi,

"Nimetoka mbali, kilichonisaidia kufika hapa nilipo ni bidii, kutokukata tamaa na kupenda kazi ninayoifa."