Nick Minaj kumlipa Tracy Champman Sh1 Bilioni kwa kosa la kutumia wimbo wake

Monday January 11 2021
nick pic

Rapa kutoka Marekani Onika Tanya Maraj maarufu Nick Minaj atatakiwa kumlipa fidia ya dola za kimarekani 450,000 sawa na zaidi ya Sh1 Bilioni muimbaji Tracy Champman kwa kosa la kutumia sehemu ya wimbo wa msanii huyo kwenye wimbo wake wa Sorry.

Minaj ambaye ametamba na ngoma kama vile Anaconda, alitenda kosa hilo mwaka 2018 ambapo alitumia sehemu ya mashairi na melodi kutoka kwenye wimbo wa Champan wa Baby Can I Hold You yanayoimbwa kwenye sekunde 30 za mwanzo za wimbo huo.

Aidha, Champan alimfungulia Minaj shitaka hilo mwaka huo huo 2018.

Hata hivyo, wimbo huo uliomuingiza Nick Minaj matatizoni haukupata bahati ya kuachiwa rasmi, lakini inadaiwa Nick Minaj aliuvujisha kwa kumpatia Dj Funkmaster Flex wa redio Hot 97 yenye makao yake Newyork Marekani ambaye alipoucheza redioni watu waliunasa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, huo sio wimho wa kwanza kwa Nick Minaj kuchanganga vipande vya ngoma za wasanii wengine hususan wa zamani, alifanya hivyo kwenye wimbo kama Super Bass, Your Love na kadhalika lakini hakuna ukiomuingiza kwehe matatizo.

Kwanini wimbo wa Champana ulimsumbua
Kwa mujibu wa Nick Minaj mwenyewe anadai alikuwa na mapenzi makibwa sana na muziki wa Champman. Hivyo wakati anatengeneza albamu yake ua Queen ya mwaka 2018 alipanga kuchanganya kipande cha wimbo wa msanii huyo kwenye wimbo wake mmoja.

Advertisement

Anadai alimtafuta Champan kumuomba lakini mama huyo ilikataa zaidi ya mara moja. Na hata walipojaribu kufanya mazungumzo na timu ya Champan jibu lilikuwa ni 'Usiurudie wimbo wangu'

Majibu hayo yalipelekea hata Nick Minaj akataka kusitisha kutoa albamu mpaka ahakikishe Champan amekubali ombi lake. Hata hivyo baadae yeye na timu yake waliamua kutupilia mbali mpango wa kuendelea kimbebembeleza Champs.

Lakini kwa upande wa Nikki Minaj binafsi aliendelea kutengeneza wimbo huo na baadae akampatia Dj Flex ambaye aliucheza redioni na sekeseke zima la madai ya hakimiliki likaanzia hapo.

Advertisement