Nandy, Harmonize kuwasha moto One Africa Music Fest Dubai leo

Friday November 26 2021
One fast PIC
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Wasanii Nandy na Harmonize ni kati ya wasanii kutoka Afrika watakapanda jukwaa la 'One Africa Musicfest' linalofanyika nchini Dubai.

Tamasha hilo linafanyika usiku wa leo Ijumaa Novemba 26 katika jiji la kitalii na kibiashara Dubai lililopo falme za kiarabu.

Tayari Harmonize ameweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionekana kashafika nchini humo tayari kuuwasha moto akiwa na mpenzi wake mpya Briana.

Tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka ndio jukwaa linaloongoza kwa hadhi zaidi katika kuonyesha vipaji bora na angavu zaidi barani Afrika, likiwa na lengo moja la kuimarisha nafasi ya Afrika katika tasnia ya burudani katika ngazi ya kimataifa

Wasanii wengine watakokuwepo katika  ukiacha Nandy na Harmonize,  ni  pamoja na Akothee na Otile Brown wote wa nchini Kenya.

Wengine ni Tiwa Savage, Wurld, Mayorku, Reekado Banks, 2baba, Dbanji, Wande Coal, Mr Flavour na Chike kutoka nchini Nigeria .

Advertisement

Wengine ni Jeff Maximum, Ruger, Skales, Dj Liya na Iphone Dj.

Advertisement