Nandy ajifungua mtoto wa kike

Staa wa muziki wa kizazi kipya Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy 'The African princess' amekiri kuuona umuhimu na ugumu wa kukamilisha kuitwa mama baada ya kujifungua katika hospital ya Aga Khan Dar es Salaam.

Msanii huyo ambae anafanya vizuri ndani na nje ya Africa Mashariki amefunguka hayo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika

"Nikisema niongee yote sitoweza, nachoweza kusema ni nakupenda sana mama maana nimeona umuhimu na ugumu wa kukamilisha kuitwa mama" amesema Nandy na kuongeza;

"Nyie ninafuraha sijawahi pata maishani mwangu nilidhani nimefurahi na mengi kumbe bado,"

Nandy ambae alifunguka hayo baada ya kujifungua mtoto wa kike na kuonyesha namna alivyofurahi na kutoa shukrani zake kwa Mungu

"Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa ukuu wake amezaliwa binti wa kichaga" amesema Nandy

Msanii huyo ambae amefunga ndoa hivi karibuni na mpenzi wake wa muda mrefu Billnas ambae ni msanii mwenzake pia wa muziki na wanatamba na nyimbo kadhaa ambazo wameshirikishana kama Bugana, Do me na Bye.