Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NA ANTI VIC: "Niliachwa na mwanamume kisa haya"

"Anti Vic, pole na majukumu ya kazi. Mimi (hataji jina lake) nimeachwa zaidi ya mara mbili na kubwa linalisababisha kufikia huku, ni tabia zangu hasa umbea. Nimeshindwa kujizuia kwenye hilo. Ndio wanawake umbea ni kazi yao lakini naona kama nimepitiliza. Natamani kurudi kwenye ndoa lakini nahofia nitamkera tena mwanamume. Nisaidie."

Anti Vic: Pamoja na mambo mengine kwenye mahusiano ya watu wengi, wanaume wengi hawapendi wanawake wambea na wanaojidai wanajua sana, kuongea sana. Ni kutokujielewa na ushamba.

Hata maandiko yanatunyima wanawake kukalia umbea na kusema watu. Kama umeolewa unatakiwa ukae na mumeo na uachane na mambo ya kuwa na mashoga kwani wanaweza hata kukaharibia ndoa yako.
Sasa wewe umejijua mwenyewe una mdomo. Unataka kurudi kwenye ndoa utaweza?

Kuna mambo mengi kama hayo. Hata hivyo, wapendwa wangu, niwadokolee tu baadhi ya mambo ambayo usipokuwa nayo makini ndoa yako inaota mbawa na kila utakapoenda utautana na 'Exit' mwanamume hatakuvumilia.

Haya hapa ni ya kuzingatia ili usiachwe na mwanamume kwani  huwa yanawakera kweli na ni ngumu kwao kuyavumilia. Jifunze hapayasije yakakukuta:


1.KUONGEA SANA
Baadhi ya wanaume na wengi wao, sio wapenda kelele. Sio waongeaji tofauti na wanawake. Wanaume ni viongozi ndani ya nyumba na kama tunavyojua, wawapo mahali na wanawake wao, wao ndio kichwa, iwe nyumbani au sehemu yoyote.

Hata hivyo, utakuta wanawake wengine kila alipo na mwanamume wake, yeye ndo mjuaji wa kila kitu. Anajibu yeye, anauliza eyeye, anashauri yeye hata kama anayetakiwa kufanya hivyo ni mwanamume.

Kwenye kelele ndio usiseme, mzozo kidogo badala ajishushe, atajidai anajua sana. Hata kama kosa ni la mwanamume, inabidi ujishushe na kufuata taratibu hata kama ni kufikia kuachana.
Mwanamke hutakiwi kuwa na sauti mbele ya mwanamume labda tu kama humpendi.

Pengine wanaume wengi huamua kukimbia nyumba zao kwa sababu ya kelele na wengine kuishia kuwaacha wanawake zao kisa kelele na kujiona waongeaji sana. Mbadilike msiachwe.


2.UCHAFU
Hapa simaanishi uchafu unaoujua wewe 'Takataka'. Hapa hadi usafi wa nafasi. Nafsi yako kama ni chafu mwanamume hawezi kuvumilia.

Sikia mwanamke. mambo ya usafi yasiwe ni sapraizi kwa mumeo. Hadi itokee mnafanya jambo fulani ndo ujiweke safi na mwenyewe ndio ashtuke 'Leo kapendeza, au leo ni msafi', hapana, muda wote mwanamke anatakiwa awe smati.

Usafi sio wa sura tu. Hata nafsi mwanamke. Unakuta mwanzo wa mahusiano, mwanamke anaonyesha uendo, kujali na hata unyenyekevu ili kumvutia mwanamume. Lakini akizama kwenye ndoa, anabadilika na hapo ndipo anapotaka mwanamume amtembue yeye ni nani. Unakosea na utaachwa mchana kweupeee!

Nani kakuambia mwanamume atavumilia hayo. Ukweli ni kwamba, wakati mwanamume anakuchagua uwe naye anajua anayoyataka na kama ukibadilika lazima agundue na atachukua tu hatua. Ndio maana unakuta wanawake wengi wanaishia kusema wameumizwa baada ya kukaa nwanamume kwa muda mrefu kumbe ni baada ya kuonyesha uchafu wake.

Tubadilike, uchafu wako usiupeleke kwa mwanamume. Pia usafi wa mwili na wengi hapa ndiyo wanafeli. Unakuta mwanamke noi mzuri lakini kwenye maungo yake ya mwisli na hasa sehemu za siri hapafai. Wanatoa harufu mbaya.

Sio huko tum, wengine wanatoa harufu mbaya kinywani, kwapani na mwili kwa jumla. Hii inakera sana kwa wanaume na unaweza usishtuke kwa nini na uzuri wako huo umeachwa kumbe jambo ni moja tu 'uchafu', mjipende.


3. UJUAJI
Ujuaji hapa simaanishi kuongea sana. Hiyo ni mada nyingine. Ujuaji hapa namaanisha mwanamke kujiona anajua kila kitu ahata ambavyo hana uhakika navyo.

Mwanamke unatakiwa ujifunze mengi kwa mwanamume wako na si kujidai kila kitu unajua hadi kuleta ushindani. Hii inakera sana wanaume na wengi huishia kuamua kukaa pembeni na kukuacha na ujuaji wako.

Kabla ya kuongea na mwamume kuhusu jambo fulani hakikisha unalitafakari na kama unajua hujui baadhi ya mambo umuulize yeye, sio kujidai mjuaji wa mambo na wakati mwingine kumkosoa hata mbele za watu.

Ni bora kunyamaza kuonekana hujui kuliko kujidai unajua na kuaharibu mambo.

Niwafichulie tu, mwanamume anapenda ku7wa na mwanamke ambaye atamfundisha mambo mengi na sio anayejua mambo mengi. Hata wanaume wasomi, wengi wanapenda kuoa wasio wasomi ili kuwafundisha kwani wanaamini ni haki yao kujifunza kutoka kwao na hiyo humfanya mwanamume ajione kweli kiongozi. Mwenzange unafanya hivyo? Badilikeni.


4. MARAFIKI
Hakuna mtu asiye na marafiki. Wanawake kuwa na marafiki wa kiume na wanaume kuwa na rafiki wa kike, ni kawaida mbona. Sema sasa  wingi wao ndiyop hadi kunamfanya mtu aone kero.

Inawezekana una marafiki wengi Mwanamke, sio mbaya lakini kuna mipaka ya kuwa na marafiki unapokuwa na mwanamume wako. Iwe kwenye uchumba au ndoa.

Tena kwenye ndoa ndiyo kabisaa, unatakiwa ikiwezekana uwafute wengi wao ubaki na wale muhimu. Hii itasaidia pia kuitunza ndoa yake.

Kingine ni mwanamke kuwa na marafiki wengi wa kiume. Hili jambo linavuruga sana wanaume wengi na wengine huona wapo kwenye mchezo wa kunyang'anyana mwanamke na kuishia kusema imetosha, kumbe wala hukumaanisha hivyo.

Sasa kwa nini uachwe bila sababu za msingi. Kwa nini umkere mwenza wako kwa kuwa na marafiki wengi wa kiume. Badilika. Kuwa na marafiki haikatazwi lakini wengi inakera, tena pale kwa kujionyesha wazina wakati mwingine kuonyesha unawathamini zaidi hata ya mwanamume wako.

Inawezekana pia mwanamume wako ametoka katika mmoja wa marafiki zako uliokuwa nao. Ikishafiki hatua ya kuwa naye, haimaanishi marafiki uliokuwa nao waendelee na ukaribu kwako ule waliokuwa nao, hivyo ni kwa wewe kuwaweka mbali na uhusiano wenu yasije yakakukuta.


5.KUOMBA PESA KILA WAKATI
Wanasema pesa ndio kila kitu. Wanawake wanapenda pesa, sijui pesa ndio inaleta furaha hadi kwenye uhusiano.... Ni kweli lakini unajua pia pesa inaweza ikaleta mfarakano kwenye mahusiano?

Chukua hii! Wapo wanawake watafutaji na pesa kwao sio tatizo. Ila kuna wale bila kuomba pesa hawajaishi. Wao ni kuwaza tu pakuche apige simu moja tu kutaka pesa. Utasiki 'pesa ya kusuka', mara, umeme umeisha, hujatulia utasikia nitumie nauli niende nyumbani, usisahau na ya kutolea', na mengine na mengine ya kukera. Kifupi matatizo ni mengi kuliko amani.

Ni ishara mbaya kuomba pesa. Mwanamume anaona unatamaa ya pesa. Kuna wengine ni tegemezi hadi inakera. Unakuta anashindwa hata kuisaidia familia yake hadi mwanamume ndio asaidie. Hawezi kutafuta kwa ajili ya wazazi wake anasubiri mwanamume huku akiwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Ni muhimu kubadilika. Mwanamke mpambanaji hata ndoa au uhusiano anaufaidi, wewe omba omba sasa, kwanza unaweza ukawa umekalia kutio kavu kwenye uhusiano bila kujua kwani mwanamume akikereka kwa kuomba pesa, uamuzi anaouchukua ni 'kesepa tu' na kukuacha na tamaa zako. Utalia?

Hizi sababu zote zinajenga kitu kinaitwa heshima  haya mambo ndio yanamuongezea mwanamke sifa ya kuwa mke au binti ambaye atafaa kuwa na kila mwanaume anayejielewa.

Kumbuka baadhi ya tabia ndizo zinaamua aina ya watu pia wanakuja kwetu, kama hujijali utawezaje kupata mpenzi anayejali.

Tuandikie maoni yako juu ya makala haya ya mahusiano. Nini kimekusibu wewe kwenye mahusiano yako ili tukupe ushauri na kujaribu kukurejesha kwenye mstari udumu kwenye uhusiano wako na ndoa. 0658-376417