Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mr P aibua maswali baada ya kubadili tarehe ya kuzaliwa

Muktasari:

  • Kupitia ujumbe aliouchapisha jana Jumatatu, Aprili 20, 2026 kwenye akaunti yake rasmi ya X (Twitter), Mr P alisisitiza kuwa uamuzi huo ni wa kibinafsi na akawaomba mashabiki wake kuuheshimu.

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Peter Okoye maarufu kama Mr P, ametangaza rasmi kubadilisha tarehe yake ya kuzaliwa kutoka Novemba 18 kwenda Novemba 30, bila kutoa sababu za uamuzi huo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha jana Jumatatu, Aprili 20, 2026 kwenye akaunti yake rasmi ya X (Twitter), Mr P alisisitiza kuwa uamuzi huo ni wa kibinafsi na akawaomba mashabiki wake kuuheshimu.

“Nathibitisha rasmi kuwa Novemba 18 si tena siku yangu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa. Tafadhali mfahamu kuwa sitapokea ujumbe wowote wala zawadi siku hiyo. Siku yangu ya kuzaliwa sasa itasherehekewa Novemba 30. Huu ni uamuzi wa kibinafsi, na ninathamini sana uelewa wenu,” ameandika.

Hatua hiyo ina maana kuwa sasa Mr P hatasherehekea tena siku ya kuzaliwa pamoja na pacha wake, Paul Okoye maarufu kama Rudeboy, ambaye walizaliwa siku moja.

Hatua hiyo inaendelea kuongeza sintofahamu tangu kuvunjika kwa kundi la P-Square 2016 ambapo lilikuwa linaundwa na mastaa hao ambao walitamba na ngoma kama ‘Chop My Money’, ‘Personally’, ‘No One Like U’ na nyingine nyingi.