Mke mwenzie Queen Darleen apata mtoto,Lulu naye mambo mazuri

Wednesday April 07 2021
mke mwenza pc
By Nasra Abdallah

Kuna usemi unasema wakati wa Mungu ndio wakati sahihi na ndicho kilichotokea kwa mke mkubwa wa Isihaka Mtoro ambaye ni  mume wa msanii  wa muziki wa bongo fleva,Queen Darleen, ambaye amepata mtoto.


Dada huyo ambaye jina lake halisi ni Sabra na mfanyabiashara wa nguo na vipodozi, amepata mtoto wake wa kwanza tangu afunge ndoa na mume wake huyo miaka kadhaa iliyopita.


Ujio wa mtoto huo umeelezwa na Isihaka leo Jumatano Aprili 7,2021 kupitia ukarasa wake w`a mtandano wa kijamii wa instagram kwa kuweka picha yenye tarehe ya leo na jina la mtoto Batsam Isihaka,na kushukuru kwa kusema Alhamdullilah.


Pia ameandika "Shukran mke wangu kwa zawadi hii Sabra,usikate tamaa, hakuna heshima hakuna upendo.

Isihaka alimuoa Queen Darleen Desemba,2019 ndoa ambayo  ilizua gumzo huko mitandaoni kutokana na msanii huyo kutowahi kuonekana kuwa katika mahusiano.

Wakati Isihaka na mkewe mambo yakiwa hivyo, upande wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael,mambo ni mazuri baada ya kuonekana kuwa na ujauzito.

Advertisement

Ujuzito huo wa lulu umeonekana kupitia mtandao wa sherehe yetu, ambapo mama wa msanii huyo na watu wake wa karibu walikwenda kumtunza vitu vya kiasili ikiwa ni siku chache tangu atoke kufunga ndoa na mfanyabiashara Francis Ciza maarufu kwa jina la Majizo.

Lulu aliyekuwa amevalia gauni pana wakati wa kupokea wageni hao, alionekana kuwa na mabadiliko katika eneo lake la tumboni.

Advertisement