Meya Dar ahoji Diamond Platnumz anakwama wapi kumuoa Zari

Wednesday June 02 2021
zari pic
By Nasra Abdallah

Meya wa jiji la Dar es Salaam,  Omar Kumbilamotoahoji msanii Diamond Platnumz anakwama wapi katika kumuoa Zari.

Kumbilamoto amehoji hayo leo Jumatano Mei 2,2021 katika hafla ya ugawaji wa taulo za kike kwa shule za msingi na sekondari  za jiji hilo, zinazotolewa na kampuni ya Keds ambapo Zari ni balozi wao na ni mmoja ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Meya huyo ambaye naye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa, amesema wakati Zari anawasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Zanaki, ambapo shughuli hiyo imefanyika,alishangaa kuona watoto wote wanamkimbilia na kuwaacha wao.

Amesema jambo linaloonyesha wazi kuwa mjasiriamali huyo ambaye amezaa watoto wawili na Diamond, ni kipenzi cha wasichana na watoto,na hajui wapi Diamond anakwama hamuoi hadi leo.

"Kwa kweli nimeshangaa, watoto wametuacha hapa kama wageni na kumkimbilia Zari,hii inaonyesha namna gani mama huyu ni kipenzi kikubwa cha watoto na mabinti zetu,Zari tunaomba ukubali Diamond akuoe.

"Nani wanataka hapa Diamond amuoe Zari, naona wote mmenyoosha mkono, tafadhali Zari sauti ya wengi ni sauti ya Mungu tunaomba tu ukubali kuolewa na Diamond,"amesema Kumbilamoto.

Advertisement
Advertisement