Meneja wa Hermonize azidi kujitanua

Wednesday September 08 2021
pua pic
By Thomas Ng'itu

ALIYEKUWA meneja  wa msanii Harmonize, Joel Joseph ‘Mr Puaz’  ameanza kujihusisha na baishara ya kuuza nguo za jinsia zote.

Puaz amesema hiyo ni mojawapo ya ujasiriamali na yeye kama mfanyabiashara hawezi akawa anategemea biashara moja.

“Ujasiriamali ni mpana sana  na lazima uwe na vyanzo tofauti tofauti vya kuingiza kipato na zaidi mimi napenda biashara sana sana iwe ni ya bidhaa au ya huduma,” amesema Puaz.

Puaz amesema licha ya kuanza kujihusisha na biashara zingine bado hajaacha kuwameneji wasanii wa muziki.

“Kuhusu suala la kusimamia wasanii hili lipo bado kwenye mchakato wangu na ni moja pia ya biashara zangu, kwa sasa najikita zaidi katika biashara ya bidhaa  na nina matarijio makubwa sana ya kuwa na brandi zangu mwenyewe zikiwemo za nguo, viatu, pochi, mafuta ya kujipaka , miwani na nyinginezo nyingi,” amesema Puaz.

Advertisement