Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchumba mpya wa Shilole, mambo hadharani

Muktasari:

  • Licha ya wawili hao kuvishana pete ya uchumba Desemba 24, 2024 wamekuwa na maisha ya siri na hawawekani mtandaoni na kwa muda mrefu mashabiki wamekuwa na hamu ya kumwona mwanamume huyo.

BAADA ya kumficha kwa muda mrefu, hatimaye sura ya mchumba mpya wa Zuwena Mohamed 'Shilole' imeonekana kwa baadhi ya mashabiki waliokuwa na hamu ya kumjua.

Licha ya wawili hao kuvishana pete ya uchumba Desemba 24, 2024 wamekuwa na maisha ya siri na hawawekani mtandaoni na kwa muda mrefu mashabiki wamekuwa na hamu ya kumwona mwanamume huyo.

Shilole amefichua ameamua kubadilisha mtindo wake wa maisha ya mapenzi na sasa hataki kuyaweka hadharani kama ilivyokuwa kwa mahusiano yake ya nyuma.

Huu ni uhusiano wa nne kwa Shilole baada ya awali kuwa na ndoa ikiwamo na Uchebe na wote alikuwa akiwaposti mitandaoni, lakini kwa huyu wa sasa Rich, amekuwa akimposti lakini bila ya kumwonyesha sura.

Mwanaspoti liliinasa picha ambayo baada ya kupostiwa ilielekezwa kwenye akaunti ya Rich na hapo pia mashabiki ndipo walipoujua ukweli.

"Kama unavyonijua mimi sina muda wa kupoteza, natoa chuma naweka chuma… lakini safari hii nimeamua mambo yangu ya mapenzi yawe siri, nimejifunza sana kuweka kila kitu binafsi mtandaoni hutokea madhara,” amesema Shilole.

Picha ya Rich iliyopatikana Instagram imeanza kusambaa na hivyo mashabiki kumjua mwanamume huyo ambaye kimwonekano ni mtulivu, mwenye mwili wa kawaida, nadhifu kwenye mavazi na anayependelea maisha ya siri.

Pia inaelezwa Rich si mtu wa mitandao ya kijamii, jambo ambalo limechangia zaidi uhusiano wao kubaki wa faragha na mbali na macho ya umma.

Wakati alipovishwa pete, ndipo uhusiano wao ulipoingia rasmi katika vyombo vya habari na sherehe ilifanyika kwenye mgahawa wa Shishi Food uliopo Kijitonyama, Dar es Salaam.Katika tukio hilo, Rich alisema hadharani  anataka kumfanya Shilole awe wa halali kwake kwa kumvisha pete ya uchumba, kauli iliyopokelewa kwa shangwe kubwa na wageni waliohudhuria, huku Shilole akipokea kauli hiyo kwa mshangao na kusema yupo tayari kuingia katika hatua mpya ya maisha ya mapenzi.

Hii ni mara ya nne kwa Shilole kuvalishwa pete ya uchumba akiwa katika maisha yake ya umaarufu, lakini tofauti na zote zilizopita, safari hii uhusiano wake na Rich unaonekana kuwa wa kimya zaidi na wenye usiri mkubwa, hali inayoendelea kuzua mjadala mitandaoni.

Hata hivyo, pamoja na kuonekana katika sherehe hiyo, lakini mashabiki wengi hawakumwona na wamekuwa na hamu ya kumjua kabla ya mambo kuwa hadharani baada ya chapisho hilo linaloendelea kusambaa mitandaoni.